Friday , 1 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Silinde achukua fomu Tunduma, atuma salamu Chadema
Habari za Siasa

Silinde achukua fomu Tunduma, atuma salamu Chadema

Spread the love

ALIYEKUWA mbunge wa Momba kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), DAVID Silinde amechukua fomu ya kugombea ubunge Tunduma Mkoa wa Songwe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Silinde amechukua fomu hizo leo Jumanne tarehe 14 Julai 2020. Hadi mchana, wagombea 16 walikuwa wamekwisha chukua fomu kuwania nafasi hiyo.

Jimbo la Tunduma lilikuwa linaongozwa na Mbunge wa Frank Mwakajoka wa Chadema.

Soma zaidi hapa

David Silinde ajiuzulu

MwanaHALISI Online limezungumza na Silinde ambaye amesema, “nimepokelewa vizuri na uongozi wa wilaya na kupewa fomu” huku akisema Chadema hakiwezi kushinda Tunduma katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020.

“Mimi kama mwanachama mpya, nitafuata taratibu zote kulingana na katiba, kanuni na mwongozo na ikiwa nitapitishwa au mtu yoyote kati yetu atapitishwa tutamuunga mkono,” amesema Silinde

“Tutaendesha kampeni za kistaarabu. Sisi kama chama tumejiandaa kushinda Tunduma na sioni kama Chadema wakishinda,” amesema Silinde ambaye amekuwa mbunge kwa miaka kumi mfululizo

 

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mwili wa Hayati Mwinyi kuagwa leo saa 8 Uwanja wa Uhuru

Spread the loveMWILI wa Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi unatarajiwa kuagwa kuanza...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi kuzikwa Machi 2 visiwani Unguja

Spread the loveMWILI wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania,...

Habari za SiasaTangulizi

Rais mstaafu Mwinyi afariki dunia

Spread the loveRais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, Ally Hassan...

Habari za Siasa

Waziri mkuu Ethiopia atua Tanzania

Spread the loveWaziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia,...

error: Content is protected !!