June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Silaha zilizoporwa Stakishari zanaswa

Kamishna wa Polisi mstaafu Suleiman Kova, ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu wa Simba

Spread the love

JESHI Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani limefanikiwa kukamata Bunduki kumi na tano na fedha taslimu za kitanzania Milioni 170. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Aidha, Silaha hizo ni zile zilizoporwa na watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi baada ya kuvamia kituo cha Polisi Stakishari Julai 12 mwaka huu Jijini Dar es Salaam na kusababisha kuuwa watu saba wakiwemo askari wanne na raia watatu.

Bunduki hizo zilikamatwa katika kijiji cha Mandimkongo Kata ya Bupu, Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani katika msitu, ambapo walikamata risasi 28 ambazo zilitambuliwa kuwaa ni moja kati ya zilizoibwa katika kituo cha staki shari.

Akielezea tukio la kukamatwa kwa silaha hizo juzi, Kamishna wa Polisi Kanda maalumu Dar es Salaam Suleiman Kova amesema, silaha na pesa hizo zilikutwa zikiwa zimefukiwa chini ya ardhi msituni humo.

Mbali na hilo, Kova amesema, Julai 17 mwaka huu kulitokea tena tukio lingine likihusisha majambazi watano ambao walihusika katika uvamizi wa kituo cha sitaki shari, ambao walikuwa wanajiandaa kuvamia maeneo ya Tuangoma wilaya ya Temeke.

Amesema, baada ya taarifa hizo kuvuja, Polisi walifanikiwa kuwadhibiti kwa majibizano ya risasi na kufanikiwa kuwakamata majambazi wawili wakiwa hai na watatu wakiwa wamefariki ambapo pia waliwakamata na risasi zilizoibiwa kituo cha sitaki shari.

Akitaja majina ya waliofariki kwa majibizano ya risasi kuwa ni, Abbas Hashimu mkazi wa Mbagala, Yasini mkazi wa kitunda, Said mkazi wa kitunda kivule, na waliopona ambao wapo chini ya ulinzi ni, Ramadhani Utale(15) mkazi wa mkuranga, Amour (24) mkazi wa mbagala kimbangulile.

Katika matukio hayo yote Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata pikipiki zipatazo nne, ambazo ni, Mc 502 yenye namba za usajili AKL –Sanrg, Mc 504, ABN-Kinglion, Mc 519, ASR-Boxer,na Mc 814- ABU-Boxer ambazo zilitumika katika uhalifu.

“Operesheni hii ni endelevu bado tunaendelea na msako hadi tutakapo hakikisha wote wanakamatwamaana silaha zilizokamatwa sio zote ambazo ziliibiwa katika kituo cha sitakai shari wanaisha kwa kuwa Jeshi letu liko makini kwa kushirikiana na wananchi”

Hata hivyo, watuhumiwa hao ambao wapo chni ya ulinzi wamewataja viongozi wao katika matukio hayo tofauti ambao wapo saba wakiwa na vyeo tofauti katika makundi hayo.

Kova amewataja viongozi hao wanaotafutwa kuwa, Abdulazizi Abdulrashid, ambae ni ostadh anayeishi Dar es Salaam-kiongozi wao, Shabani Matumbuka maarufu kama, Amir Shaban Ndobe,Hannafi Kapela –Shekh Hannafi, Hassan Issa maarufu kama Dk. shujaa, Zahaq Ngai, maarufu kama Mtu mzima.

Wengine ni, Abubakar Ngindo maarufu kama Abu Muhammad, Khamis Ramadhani na Ustadhi Rashidi ambae aliuawa katika tukio la sitakishari, ambapo iliuliwa na wenzake ili kupoteza ushahidi.

“Nitoe wito kwawananchi wote wenye kuwatakia mapenzi mema nchi yetu waendelee kutoa taarifa kw kila hali ili kuweza kukomesha janga hili. Lakini pia niwatoe hofu wnanchi wae na amani kwani Jeshi la polisi liko kwenye mapambano makubwa ya kuhakikisha hali inakuwa shwari” amesema Kova,

error: Content is protected !!