Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Silaha za kivita zakutwa kwenye gari lililomteka Mo
Habari Mchanganyiko

Silaha za kivita zakutwa kwenye gari lililomteka Mo

Spread the love

MKUU wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro amesema silaha ya kivita aina ya AK-47, pisto tatu pamoja na risasi 19 zimekutwa katika gari lililotumika kumteka Mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 20 Oktoba 2018, IGP Sirro amesema polisi baada ya kufanya ukaguzi ndani ya gari hilo aina ya Toyota Surf ambalo lilitelekezwa usiku wa kumkia leo na wanaodaiwa kumteka Mo Dewji, wamekuta silaha hizo hatari.

IGP Sirro ameeleza kuwa, kutokana na hatari ya silaha hizo, watekaji hao kama wangefanikiwa  kutoroka na Mo Dewji nje ya nchi ingekuwa hatari zaidi.

“Katika upekuzi ndani ya gari tumekuta sialaha nne, silaha ya kivita na kuna uwezekano wametoka nayo kwao na pisto tatu. Baada ya kufanya ukaguzi Mohamed alitekwa kwa silaha nne, ni hatari sana na kama wangetoroka naye ingekuwa shida sana, risasi 19 za kivita na silaha ambazo unaweza piga mfululizo,” amesema IGP Sirro.

IGP Sirro amesema watekaji hao  baada ya kuona kwamba hawawezi kutoroka nje ya nchi kutokana na uwepo wa ulinzi mkali, waliamua kuliterekeza gari hilo. Na kwamba kama wangechelewa kidogo Jeshi la Polisi lingewakamata.

“…Hii gari imetelekezwa hapa Mo akawa ameachiwa lakini ameeleza kwamba watu hawa walikuwa wanahitaji fedha, fedha kiasi gani hawakusema, lakini anasema walikuwa na wasi wasi sana, wanahoji wakiwa na wasi wasi wakiwa na silaha zao.

Walipotoka Colosseum walikwenda moja kwa moja kumpeleka chumbani,  aliwapa simu ya baba yake wazungumze nae lakini kwa sababu ulinzi wetu ulikuwa imara wakawa wanaogopa  kuwasiliana na wazazi wake,” amesema IGP Sirro.

Katika hatua nyingine, IGP Sirro amesema Jeshi la Polisi limebaini mtandao uliohusika kumteka Mo Dewji ambao wahusika wametoroka kurudi nchini mwao.

Mo Dewji mfanyabiashara maarufu ndani na nje ya nchi ambaye pia ni muwekezaji katika klabu ya Simba, alitekwa alfajiri tarehe 11 Oktoba katika hoteli ya Colosseum iliyoko maeneo ya Oesterbay  jijini Dar es Salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awataka wahariri kufanya kazi bila uoga, upendeleo

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amewataka wahariri wa vyombo...

Habari Mchanganyiko

STAMICO yasaini mkataba wa bilioni 55.2 kuchoronga miamba GGML

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limezidi kufanya vizuri katika...

Habari Mchanganyiko

NMB yatoa traksuti za Mwenge wa Uhuru Mtwara

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa traksuti kwa mkoa wa Mtwara ambako...

Habari Mchanganyiko

Yara yaja na bima ya mazao kwa wakulima

Spread the love  WAKATI serikali ikiweka mikakati mbalimbali kuimarisha sekta ya kilimo...

error: Content is protected !!