Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Siku ya wahasibu duniani yafana Dar
ElimuHabari

Siku ya wahasibu duniani yafana Dar

Mwenyekiti wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu za Serikali (NBAA), Profesa Sylivia Shayo katikati akiwakaribisha wageni wengine kwenye maadhimisho ya Siku ya Wahasibu Duniani iliyoandaliwa na Chama cha Wahasibu Wanawake Tanzania (TAWCA). Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA CPA Pius Maneno
Spread the love

WAHASIBU na Wakaguzi wa Hezabu nchini wametakiwa kuweka mbele maslahi ya umma, kuwa waadilifu na kuzingatia maadili na sheria zinazowaongoza kwenye kazi zao za kila siku zza kihasibu. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Wito huo ulitolewa Alhamisi na Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu za Serikali (NBAA), Profesa Sylivia Temu, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wahasibu Duniani.

“Tuzingatie uzalendo na maslahi ya taifa lakini pia nimewaasa tusijifungie kwasababu dunia imekuwa kama kijiji hivyo tujipange tuwe na mtazamo mpana ili tuweze kufanyakazi za kimataifa kama Umoja wa Mataifa,” alisema

“Nimewaambia wahasibu kwamba tumeshaandika hadithi ya miaka 50 iliyopita sasa tujiulize miaka 50 ijayo tunafanya nini ili tuwe endelevu tusiwe wale wale tu tunatakiwa kwenda sanjari na mabadiliko,” alisema

Aidha, alisema bodi ya NBAA imeshaanza kuonyesha mfano kwa kufanya kazi za kihasibu kimataifa ambaapo wameanza kutoa ushauri nchini Msumbiji na Malawi na wanatarajia kwenda kwenye mataifa mengine.

Baadhi ya wageni wakifuatilia mada mbalimbali kwenye maadhimisho ya Siku ya Wahasibu Duniani yaliyofanyika Alhamisi Posta jijini Dar es Salaam yaliyoandaliwa na Chama cha Wanawake Wahasibu Tanzania (TAWCA)

Alisema wahasibu na wakaguzi wanapopata kazi za kimataifa wasizikatae kwani zitailetea heshima nchi na  wahasibu wa Tanzania watapata sifa kwa umahiri na ubobezi kwenye fani hiyo na pia itawaongezea uchumi.

Aliwataka wahasibu na wakaguzi wapambane kuikuza taaluma yao katika nyanja ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kwenda na kasi ya teknolojia duniani.

“Tukiachwanyuma kiteknolojia nirahisi watu wengine wakafanyakazi ambazo siyo za uadilifu kwa kutumia teknolojia hiyo lakini sisi tukiwa vizuri kweneye teknolojia tutaweza kusimamia vizuri rasilimali fedha,” alisema

Alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumteua kuwa mwenyekiti wa bodi wa kwanza mwanamke wa bodi hiyo kwa miaka 52 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1972.

“Namshukuru kwa kuniamini na muahidi kwamba nitafanya kazi na wenzangu kwa uaminifu mkubwa kuhakikisha fani hii inafanyika kwa uadilifu mkubwa,” alisema

Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA, CPA Pius Maneno alisema maadhimisho hayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka na sherehe hizo mwaka huu zinaenda sanjari na maadhimisho ya miaka 50 ya NBAA iliyoanzishwa 1972.

Alisema NBAA imefanya mambo mengi kuongeza idadi ya wahasibu nchini ambao kwa sasa wako zaidi ya 26,000 na imefanya ukaguzi kwenye makampuni 450 kuangalia kama yanafuata matakwa ya sheria.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu za Serikali (NBAA), Profesa Sylivia Shayo, akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Wahasibu Duniani iliyoandaliwa na Chama cha Wahasibu Wanawake Tanzania (TAWCA).

“NBAA imeongeza idadi ya watahiniwa kwasasa mitihani  ambayo inafanyika Novemba au Mei kunakuwa na wanafunzi kama 7,000 wanaofanya mitihani hiyo na tumetoa miongozo mbalimbali,” alisema ,

Alisema miongoni mwa mafanikio ya NBAA ni nchi mbalimbali kuja kujifunza namna ya kufanya kazi za kihasibu kwani kwa sasa NBAA inamkataba wa miaka mitano na serikali ya Msumbiji kufundisha masuala y uhasibu na fedha kwenye sekta ya umma.

Alisema kwa miaka hiyo 50 NBAA imefanikisha kuwa na majengo yake yenyewe na akuwa na kituo cha Wahasibu Bunju APC na kwamba wamekutana kwenye maadbhimisho hayo wahasibu wa zamani na wa sasa kubadilishana mawazo namna ya kuboresha taaluma.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu za Serikali (NBAA), Profesa Sylivia, akiwaongoza wageni mbalimbali waliofika kwenye maadhimisho ya Siku ya Wahasibu Duniani yaliyoandaliwa na Chama cha wahasibu Wanawake Tanzania TAWCA.

“Kikubwa tumeambiana tufanye kazi kwa uadilifu na kwa kufuata taratibu miaka 50 ijayo tuendeleze matumizi ya TEHAMA na kwa sasa shughuli zote za NBAA zinafanyika kwa TEHAMA kasoro usimamizi wa mitihani pekee,” alisema CPA Maneno

Alisema kutokana na kufanya vizuri kwenye sekta ya uhasibu Afrika imeitambua Tanzania kwamba inaongoza kwa usimamizi mzuri wa fedha kwenye sekta ya umma na ndiyo sababu ripoti ya Shirikisho la Wahasibu Duniani mwaka 2021 imeonyesha Tanzania na Nigeria ndizo zimefikia ubora wa viwango vya uhasibu vya kimataifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanawake GGML wawanoa wanafunzi Kalangalala Sec. kujitambua

Spread the loveKATIKA kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, Umoja wa...

ElimuHabari Mchanganyiko

RC Songwe ang’aka kesi 2 kati ya 60 za mafataki kuamuliwa

Spread the loveMkuu wa mkoa wa Songwe Dk. Fransis Michael ameshangazwa na...

error: Content is protected !!