July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Siku ya uchaguzi yamponza waziri

Wananchi wakiwa kwenye foleni ya kupiga kura

Spread the love

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Jenister Mhagama, amepata wakati mgumu alipokuwa akitetea kuwa, siku ya Jumapili haiwezi kubadilishwa kuwa ya kupiga kura hadi pale Tume ya Uchaguzi itapapokuwa imekubali mapendekezo. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Mhagama ametoa utetezi huo, alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Nkenge, Assumpter Mshama (CCM), aliyetaka kujua ni kwanini Serikali isishirikiane na NEC kubadilisha siku hiyo inayoangukia Jumapili kila uchaguzi.

Majibu hayo yalionekana kumkera mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe (CCM), ambaye amesema ana mashaka kuwa Mhagama anaweza kuwa sio mcha Mungu na kutaka kujua yeye ni dini gani kama sio Mkristo.

Katika swali lake, Filikunjombe amesema amesikitishwa na majibu ya Mhagama kwamba uchaguzi utafanyika Jumapili.

“Sisi wabunge humu ndani tulishakataa uchaguzi usifanyike Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kwa sababu watu wanakwenda kusali na ili uchaguzi uwe na ufanisi zaidi.

“Bunge ni chombo cha mwisho, Tume ya Uchaguzi haiwezi ikawa juu ya Bunge. Mbona wenzetu Malawi wanafanya uchaguzi Jumatatu kwa nini na sisi tusifanye siku hiyo ili na wewe ukasali? amehoji Filikunjombe.

Akijibu swali hilo, Mhagama amesema yeye ni Mkristo na imani yake haiwezi kubadilika kwa sababu yoyote ile. Kwamba, Katiba ya Jamuhuri ya Muungano, Ibara ya 74 (7) imetoa maelekezo kwa Tume ya Uchaguzi itakuwa huru, hivyo ndiyo yenye mamlaka ya kupanga siku ya uchaguzi.

“Kutokana na mamlaka hayo, Tume inaendelea kupokea maoni ya wadau mbalimbali na kama ikiona inafaa itapanga siku nyingine kwa ajili ya uchaguzi,” amesema.

Awali akijibu swali la msingi la Mshama, Mhagama amesema bado Watanzania wataendelea kuitumia siku ya Jumapili katika kupiga kura kwenye chaguzi zake.

Mhagama ameongeza kuwa uchaguzi unafanyika kwa mujibu wa ibara ya 74 ya Katiba kifungu 6 mpaka 15 ambavyo vimeipa Tume ya Uchaguzi madaraka ya
kuratibu na kusimamia uchaguzi.

Amesema bado serikali haijafanya utafiti ili kujua kama inaweza kupoteza kitu chochote ikiwa itafanya mabadiriko ya kuondosha siku hiyo na kupanga siku nyingine yoyote.

error: Content is protected !!