May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Siku nne za Papa Francis Iraq

Spread the love

 

ZIARA ya siku nne ya Papa Francis, Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, nchini Iraq, zimehitimishwa leo Jumatatu tarehe 8 Machi 2021, huku ujumbe wa amani ukitawala. Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea).

Katika siku hizo, Papa Francis (84) ametembelea mikoa mitano ya nchi hiyo, ambapo kila alipopata wasaa, alihubiri umuhimu wa amani na upendo duniani.

Ziara yake ilianzia katika Mji wa Kistoria wa Najaf uliopo Kusini mwa taifa hilo, kwenye mkutano huo, alikutana na kiongozi wa Waislamu wa madhehebu ya Shia, Ayatollah Ali al-Sistani.

Baada ya mazungumzo ya amani na kiongozi huyo, alitembelea eneo la Nineveh lililopo Kaskazini Iraq ambapo alizungumza na Wakristo waathirika wa mapigano kutoka kundi la uasi la Dola ya Kiislam (IS).

Katika mazungumzo na Wakristo hao, Papa Francis aliwaeleza lengo la ziara yake kwamba, ni kutafuta amani na mshikamano duniani.

Siku ya pili, ya ziara yake, Papa aliwakutanisha Wakristo katika Kanisa la Mtakatibu Joseph Chaldean lililopo katikati mwa Baghdad akiwa na ujumbe ule ule.

Siku ya tatu, Papa Francis alitembelea eneo la kaskazini mwa Iraq ambalo wakati mmoja lilikuwa likishikiliwa na wanamgambo wa IS..

Wakristo walikua miongoni mwa watu waliolengwa na IS wakati walipoteka eneo hilo mwaka 2014, na kutekeleza ukiukwaji wa haki za binadamu.

Kisha Papa amehitimisha kwa Ibada ya Misa katika uwanja wa mpira mjini Irbil, iliyohudhuriwa na maelfu ya watu.

error: Content is protected !!