April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Siku nane za Mbowe, wenzake kujinasau kizimban

Spread the love

VIONGOZI tisa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wanatarajiwa kuanza kujitetea kwa siku nane mfululizo. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Ni katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kupatikana na kesi ya kujibu kwenye kesi namba 112/2018 yenye mashtaka 13 ikiwemo uchochezi.

Viongozi wanaoshtakiwa kwenye kesi hiyo ni Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema-Taifa; Dk. Vicent Mashinji, Katibu Mkuu; John Mnyika, Naibu Katibu -Bara; Salum Mwalimu, Naibu Katibu -Zanzibar.

Wengine ni Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini; Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini; Jonh Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini; Ester Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini; Halima Mdee, Mbunge wa Kawe.

Mawakili wanaowatetea ni Prof. Abdallah Safari, Peter Kibatala, Jeremiah Mtobesya, Hekima Mwasipu, John Mallya, Frederick Kihwelo na Dickoson Matata.

Upande wa Mashtaka (serikali) unawakilishwa na Faraja Nchimbi, Wakili wa Serikali Mkuu; Dk. Zainab Mango, Wakili wa Serikali Mkuu; Wankyo Simon, Wakili wa Serikali Mwandamizi na Jackline Nyantori, Wakili wa Serikali.

Utetezi wa Mbowe na wenzake ulitarajiwa kuanza tarehe 17 Septemba 2019 ambapo Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba aliamua kuahirisha baada ya upande wa washtakiwa kudai kuwa, Mchungaji Msigwa na Heche wamepata msiba wa ndugu zao wa karibu.

Hakimu Simba aliikataa hoja ya kuwa, wakili muungoza jopo, Prof. Safari alikwenda kwenye mashauri ya mahakama kuu, kanda ya Shinyanga mbele ya Jaji Cypriani Mkeha na Wakili Kibatala kwenda mahakama kuu kwa wito wa hati ya kuhudhuria shauri.

Pia alipinga Wakili Mwasipu kuhudhuria kesi ya mahakama kuu, kanda ya Tanga kwa kuwa, bado kuna mawakili wengine wengeza kuwawakilisha watuhumiwa hao.

Hakimu Simba amepanga kuanza kusikiliza utetezi wa washtakiwa kuanzia tarehe 24 Septemba 2019, siku ya Jumanne hadi tarehe 27 Septemba 2019.

Pia shauri hilo limepanga kusikiliza tarehe 1 Oktoba 2019 hadi tarehe Oktoba 2019 (Jumanne-Ijumaa).

Hakimu Simba amesisitiza kuwa anataka kulimaza shauri hilo haraka, kwa kuwa lina mwaka na miezi takribani sita.

Kwenye shauri hilo, Mbowe na mwenzake wanashtakiwa kufanya maandamano yaliyokinyume cha sheria, kutoa maneno ya uchochezi na kusanyiko haramu lililosababisha kuuawa kwa Mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwelina Akwilini.

error: Content is protected !!