January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Siku 75: Morris, Mudathir warejea tena Azam, Sure Boy…

Aggrey Morris

Spread the love

 

SIKU 75 za wachezaji waandamizi wa vijana wa rambaramba Azam FC ya jijini Dar es Salaam, kukaa kifungoni zimemalizika na kurejea mazoezini kuungana na wenzao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Wachezaji hao waliosimamishwa kwa muda usiojulikana kuanzia tarehe 6 Oktoba 2021, kwa utovu wa nidhamu walikuwa ni nahodha Aggrey Morris, nahodha msaidizi Salum Abuubakar ‘Sure Boy’ na kiungo Mudathir Yahya Abbas.

Jana Jumatatu, tarehe 20 Desemba 2021, ikiwa ni siku ya 75 tangu walipokosenana uwanjani, wachezaji hao, walionekana tena katika uwanja wa mazoezi isipokuwa Sure Boy.

Morris ambaye ni mchezaji mwandamizi ndani ya viunga vya Chamanzi na Mudathir walikuwa wakipasha na wenzao.

Mudathir Yahya Abbas (kushoto)

Tetesi zinazoendelea kwa kipindi cha wiki mbili sasa ni kwamba, Sure Boy yupo mbioni kujiunga na Yanga ya jijini Dar es Salaam.

Katika kipindi chote hicho, Azam FC imekuwa ikipata matokeo yasiyoridhisha ikiwemo kufungwa na kutoka sare katika michezo ya ligi kuu Tanzania Bara 2021/22.

Kati ya michezo tisa iliyokwisha kucheza, imejikusanyia pointi 12 ikiwa nafasi ya nane mbele ya vinara wa ligi hiyo Yanga ya jijini Dar es Salaam, yenye pointi 23 sawa na michezo tisa iliyocheza.

Matokeo hayo yakusuasua, yalimfanya kocha wake mkuu, George Lwandamina akitangazakujizulu nafasi yake.

error: Content is protected !!