Spread the love

 

KLABU ya Soka ya Yanga ndani ya siku 17 zijazo, huwenda ikamaliza mchezo kwa kutangazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara kwa mara ya 28 katika historia yao. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Vinara hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara wamejinasibu hivyo mara baada ya kwenda sare ya bil;a kufungana, dhidi ya Ruvu Shooting kwenye mchezo uliopigwa kwenye dimba la Lake Tanganyika, Kigoma.

Akizungumza na chombo kimoja cha habari mara baada ya timua ke kwenda sare, Afisa Habari wa klabu ya Yanga Hassan Bumbuli alisema kuwa matokeo hayo kwa klabu ya mpira wa miguu ni kawaida, kwani kila siku hauwezi kupata matokeo unayoyata.

“Kwenye mp[ira wa Miguu matokeo hayo ni kawaida sana kwa kuwa mpira unamatokeo matatu na sisi tumepata mmoja ya tokeo kati ya hayo.” Alisema Afisa Habari huyo

Matokeo hayo dhidi ya Ruvu Shooting, inaifanya Yanga kupata sare tano mpaka sasa katika michezo 22 waliocheza huku wakishinda michezo 17, nakuendelea kushika rekodi ya kuwa timu pekee kati ya 16 zinazoshiriki Ligi msimu huu kutopoteza mchezo wowote.

Akizungumza juu ya matarajio ya ubingwa, Bumbuli alisema kuwa suala la ubingwa bado lipo palepale na kuwahakikishia mashabiki wa timu hiyo kuwa nadni ya mwezi huu Mei kuisha basi lengo hilo litakuwa lishatia.

“Ubingwa upo palepale na nikuhakikishie tu na nikiongea huku najiamini, kabla ya mwezi huu kuisha tutakuwa tumeshamaliza hiyo kazi na pengine itabakia kutuambia wapi watatukabidhi kombe letu.” Alisisitiza Bumbuli.

Yanga mpaka sasa imebakisha michezo nane ili kuhitimisha mbio katika msimu huu, ambao umeonekana bora kwa upande wao kufuatia kupata matokeo mazuri katika michezo yao.

Katika michezo hiyo nane, michezo mine wataicheza ndani ya mwezi huu wa Mei, huku kati ya hiyo miwili watakuwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa.

Kwenye kutekeleza malengo yao kwa mwezi huu, Yanga itaana kushuka dimbani Mei 9 mwaka huu dhidi ya Tanzania Prision kwenye mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, majira ya saa 1 usiku.

Mara baada ya mchezo huo Yanga itafunga safari mpaka jijini Dodoma, ambapo Mei 15 mwaka huu itashuka dimbaji Jamhuri kumenyana na Dodoma Jiji, majira ya saa 10 jioni.

Vinara wa Ligi hiyo kwa mwezi Mei hawatoishia hapo, Mei 21, watakuwa tena kwenye dimba la nyumbani dhidi ya Mbeuya Kwanza majira ya saa 1 kamili usiku.

Ratiba ya mwezi Mei kwa Yanga itatamatika kwa kusafiri mpaka jijini Mwanza kwenye dimba la Ccm Kirumba, kumenyana na Biashara United kutoka mkoani Mara.

Kama Yanga wakifanikiwa kushinda michezo hiyo yote mine, watafikisha alama 68, nakuhitaji alama tatu tu, waweze kutangazwa kuwa mabinga wapya wa taji la Ligi Kuu.

Kwa sasa mpinzani wa karibu wa Yanga kwenye msimamo ni klabu ya Simba ambao wapo kweenye nafasi ya pili wakiwa na pointi zao 43, huku wakiwa wamebakiza michezo tisa tu mkononi na kama wakifanikiwa kushinda yote watakuwa wamefikisha jumla ya pointi 70.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *