September 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

SIKIKA yataka majipu MSD yatumbuliwe

Spread the love

RAIS John Magufuli ameombwa kutumbua watumishi wa Bohari Kuu ya Dawa Tanzania (MSD) waliohusika kusafirisha dawa kutoka kwenye bohari hiyo kwenda katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) mwaka 2012 na kushindwa kuzifikisha ndani ya wakati, anaandika Pendo Omary.

Pia SIKIKA imeishauri serikali kuweka mfumo utakaowezesha ufuatiliaji na usambazaji wa dawa zinazotolewa katika hospitali zake ili kudhibiti ufisadi unaofanywa na watumishi wasio waminifu katika sekta ya afya,

Kauli hiyo imetolewa huku Prof. Mussa Assad, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika ripoti yake inayoishia Juni mwaka 2015 ikionesha utata katika usambazaji wa dawa kutoka MSD.

Ripoti hiyo inaonesha kuna dawa zenye thamani ya Sh. 2 Bilioni zipo jiani kutoka katika Bohari Kuu-Keko, jijini Dar es Salaam kwenda MNH tangu Mei 2012 na mpaka sasa hazijafika.

Akizungumza na MwanaHALISI Online Irinei Kiria, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la SIKIKA –linalohusika na utetezi wa masuala ya afya nchini amesema “dawa za bilioni mbili ni nyingi. Wapo wagojwa waliofariki au kutotibiwa kwa wakati kutokana na hospitali za serikali hasa Muhimbili kukosa dawa za kutosha.

“Sio kila mgojwa anaweza kununua dawa. Wagojwa wanaotibiwa kwa msamaha ndio waathirika wakubwa. Hata wahudumu wa afya kwa namna mmoja wameathirika na uzembe huu kwa sababu hawafurahii kutoa huduma bila dawa pale inapohitajika,” ameongeza;

“Kwa ujumala, waliohusika wawajibike kwa sababu CAG hakusema kama wahusika waliwajibishwa. Pia ni muhimu serikali ikaweka mifumo imara kuhakikisha dawa zinafikishwa hospitali kwa wakati.

Hata hivyo, wakati CAG akitoa taarifa hiyo tayari MwanaHALISI Online 31 Mai, 2015 ilinukuu taarifa ya SIKIKA ikisema mahitaji ya dawa muhimu na vifaa tiba yameongezeka kutoka Sh. 188 bilioni mwaka 2011/2012 hadi Sh. 577 bilioni mwaka 2014/2015 na makadirio ya Sh. 36.2 bilioni kwa mwaka wa fedha 2015/2016.

Aidha kwa miaka ya fedha 2011/2012 na 2012/2013 kulikuwa na ongezeko kubwa kidogo la bajeti ya dawa muhimu na vifaa tiba ambazo ni Sh. 123.4 bilioni na Sh. 80.5 bilioni ingawa hakukuwa na matokeo chanya ya upatikanaji wa dawa.

Miaka minne iliyopita ukiondoa mwaka wa fedha 2012/2013 ambapo fedha yote iliyoidhinishwa ilitolewa, ni asilimia 78 tu ya wastani wa fedha zinazoidhinishwa ndizo zimekuwa zikitolewa.

error: Content is protected !!