January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

SIKIKA: Tusitumike kuhalalisha sheria mbovu

Mkurugezi wa SIKIKA, Irenei Kiria

Spread the love

SIKIKA imetaka isitumike kuhalalisha upitishwaji wa Sheria za Makosa ya Mtandao na Miamala ya Kielektroniki iliyopitishwa na Bunge wiki hii. Anaandika Pendo Omary .… (endelea).

Kauli hiyo imetolewa na Irenei Kiria – Mkurugezi wa SIKIKA -taasisi inayofanya kazi ya ushawishi na utetezi wa masuala ya afya nchini.

Akizungumza na MwanaHALISIOnline leo, Kiria amesema “huko ni kulitumia jina la SIKIKA vibaya”.

Kiria amesema, “naomba nifafanue kuhusu propaganda inayoenezwa na maafisa wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia kituo cha redio cha Clounds FM katika kipindi cha Power Breakfast cha leo asubuhi, kuhusu SIKIKA na Mswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao (CyberCrime) wa mwaka 2015”.

“SIKIKA haikuhudhuria mkutano wa wadau unaodaiwa kufanyika Dodoma wala hatukutoa maoni kuhusu Mswada wa Miamala ya Kielektroniki kama inavyosemwa na Peter Serukamba – Mbunge wa Kigoma Mjini na maafisa wa TCRA,” amesema Kiria.

Kiria amesema, 29 Machi mwaka huu, SIKIKA ilituma kwa njia ya mtandao wa email “ombi kusitisha upitishwaji wa Mswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao kwa hati ya Dharura” kwa Peter Serukamba – Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu ya Bunge.

SIKIKA ilituma ombi hilo kwa niamba ya mashirika ya Change Tanzania, Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) na SIKIKA yenyewe.

Sehemu ya maoni hayo yanasomekaMuswada huu haukuwekwa wazi mpaka tarehe 29 Machi na ratiba inaonyesha muswada utapitishwa chini ya hati ya dharura tarehe 31 Machi, hivyo wananchi hatujapata nafasi ya kupitia kwa kina na kutoa maoni makini kuhusu muswada huo”.

Aidha, “muswada unalenga na kuhusisha kudhibiti mawasiliano ya wananchi wenyewe kwa wenyewe suala ambalo linaweza kupingana na katiba ya nchi sheria zilizopo na haki za binadamu za umoja wa mataifa”.

Kiria amesema maoni hayo hayakutumika kuboresha mswada huo bali kuongeza tu orodha ya wadau wanaodaiwa “kushiriki” kwa lengo la kuonesha kuridhia.

“Kwa kuwa maoni ya wadau hayakuzingatiwa na kwamba Mswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao iliyopitishwa ina mapungufu mengi, SIKIKA na wadau bado wanaipinga. Tunaomba jina la SIKIKA lisiendelee kutumika kuhalalisha upitishwaji wa sheria hii,” amesisitiza Kiria.

error: Content is protected !!