January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Si mafuriko tena, ni maporomoko

Edward Lowassa akiwasili kwenye ofisi kuchukua fomu za kuwania Urais kupitia Chadema

Spread the love

SIKU mbili baada ya kukihama chama alichokulia, Chama Cha Mapinduzi (CCM), mwanasiasa machachari nchini, Edward Lowassa, hatimaye amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea urais kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Anaandika Sarafina Lidwino …  (endelea).

Lowassa alifika makao makuu ya Chadema, yaliyopo eneo la mtaa Ufipa, Kinondoni, jijini Dar es Salaam, majira ya saa 6:44 mchana; akiwa ameongozana na mkewe Regina Lowassa.

Katika eneo la Ufipa, maelfu ya wananchi walijipanga kandokando ya barabara kumlaki kiongozi huyo. Alikabidhiwa fomu ya kugombea nafasi hiyo na Freeman Mbowe, mwenyekiti wa taifa wa Chadema.

Mara baada ya kukabidhiwa fomu ya kugombea urais, Lowassa alisema, “…mmenipa heshima kubwa. Sina cha kuliwapa zaidi ya kuwahidi, kwamba nitafanya kazi mliyonituma kwa uadilifu.”

Alisema, “…jibu la shukrani zangu, ni namna gani nitawatendea haki. Nakishukuru chama kwa mapokezi mazuri na wale wote waliojitolea pesa kwa ajili ya kununua fomu na kunikabidhi. Naamini kuwa nguvu zenu na matumaini yenu kwangu kuhusu taifa lenu yatakamilika.”

Amesema njia pekee ya kuhakikisha taifa hili linafikia malengo yake katika utawala mpya, ni kuhakikisha walio na sifa wakajiandikishe ili kupata uhalali wa kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Hata hivyo, Lowassa aliomba viongozi wa Chadema, wanachama na wananchi wengine, kushirikiana kwa pamoja ili kupatikane nguvu ya kuiong’oa CCM madarakani.

Kuhusu kashfa mitandaoni Lowassa amesema, wanaotumia muda mwingi kumkebehi kutokana na uamuzi wake wa kuhama CCM, Lowassa alisema, “…sina muda wa kuwasikiliza na wala hawataniyumbisha.”

Alisema, “Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alisema, “Wananchi wanataka mabadiliko. Wakiyakosa ndani ya CCM, watayatafuta nje ya CCM. Nimejiridhisha kuwa ndani ya CCM hakuwezi kupatikana mabadiliko. Miaka 52 ya uhuru, tumebaki palepale. Ni vema wakaachiwa watu wengine kuendesha nchi ili kuondoa umasiki wa Watanzania.”

Lowassa ambaye aliyejiuzulu uwaziri mkuu mwaka 2008 alikuwa miongoni mwa wagombea 38 waliorejesha fomu za kugombea nafasi hiyo CCM, jina lake lilikatwa katika hatua za awali kutokana na kile kilichoolezwa “kutotakiwa na mwenyekiti wa CCM.”

Hatua ya Kamati Kuu (CC), kukata jina la Lowassa kuliibua mjadala mzito ndani na nje ya CCM huku baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho (NEC), wakitoka tahadhari na kueleza kutoridhwa na uamuzi huo.

Kabla ya Lowassa kukabidhiwa fomu ya kugombea nafasi hiyo, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alisema, “tukio la leo ni la kihistoria;” na matunda ya kazi ya kitafiti ya zaidi ya miezi mitatu iliyofanywa na chama hicho.

Alisema, “Tumefanya kazi kubwa na utafiti wa kina hadi kumpata Lowasa na tulikuwa hatutaki kumtangaza mapema kwa sababu tulikuwa hatutaki kukurupuka leo tumemaliza na ndio maana tumemtangaza kwenu.”

Amesema, utafiti wa kumpendekeza Lowasa ulishirikisha viongozi wote wakuu, akiwamo katibu mkuu, mwenyekiti na naibu katibu mkuu.

“Hatukukurupuka. Tumefanya maamuzi sahihi na yalifanyika kwa kufuata katiba ya Chadema ya mwaka 2006 Ibara ya 39,1 (c).

Akiongea kwa kunukuu ibara hiyo, Lissu alisema, Lowassa ametimiza masharti yote ya lazima ya kupendekezwa kuwa mgombea urais wa Chadema na jumuiko la vyama vine vinavounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

“Kwa kuzingatia vigezo hivyo, kamati kuu imejiridhisha kwa kufanya uchunguzi na kutembelea mahakama zote nchi na kubaini kuwa, Lowasa hajawahi kushitakiwa wala kuwa na kosa lolote mahakamani.Hivyo wanachama wote wanatakiwa kuheshimu maaumuzi ya kamati kuu,” ameeleza Lissu.

Akizungumzia umuhimu wa kushinda uchaguzi, Lowassa alisema, mara baada ya kuvuka kiuzi cha kuingia katika urais Octoba 25, atakuwa na jukumu la kuteua mawaziri.

Amesema, Tumeya uchaguzi (NEC), imeongeza majimbo mapya 26 hivyo kuwa na majimbo 265. Hivyo, tunahitajika kushinda viti vya wabunge 133. Kazi kubwa ni kushinda urais pamoja na kupata wabunge wengi zaidi bungeni.

Awali Lissu alikana madai kuwa amejiuzulu nafasi yake na kusema, “…tuhuma hizo sio za kweli.”

 

error: Content is protected !!