April 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Si akili zao, ni kufilisika

Bernard Membe, Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Tanzania

Spread the love

KUFILISIKA huwa hakupigi goti. Wala anayefilisika huwa hajijui; huwa anadhani kilichopungua leo atafidia kesho. Anaandika Mwandishi Wetu … (endelea).

Mfano, mfanyabiashara wa duka, kwa kawaida hupanga bidhaa zake kwenye shelfu. Bidhaa zikianza kupungua tu, ili kuonesha bado zimejaa hupanga maboksi, na kadri anavyozidi kufilisika, hata maboksi hukosekana, shelfu zinabaki wazi.

Hata kufilisika kisiasa hakupigi hodi. Mwanasiasa akifilisika hupanga maboksi akilini mwake. Hebu kitazame Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilivyo na watu maarufu na wasomi lukuki, angalia mijadala yao – wao kwa wao wanatuhumiana, wanatukanana- huku ndio kufilisika.

Hizi sio akili zao! Chama tawala kinafurahia matusi? Wanamtunza mtu anayetukana? Tena wanatukana wazee, watoto wadogo wanapaza sauti, wanawatukani.

Ila kwa uamsho huu wa bongo mpya za vijana na mitandao ya kijamii, hawaponi. Wanaojua kukokotoa wanaweka hesabu hadharani, kuhoji kwao kunafungua masikio wananchi. Siku hazigandi, 2020 hiyo hapo.

Kama muuza duka vile, watu wanaofilisika hawajijui. Kinachowatia upofu ni mamlaka zao, wanaamini kwamba wanaweza kulazimisha mahaba kwa hadaa. Never, nasema never.

Unawezaje kuwajua watu aliyefilisika? Hujengwa na hulka kadhaa, miongoni mwao ni zile zinazowaingiza katika kundi la upofu. Huziba mishipa ya fahamu huku wasiruhusu bongo zao kutawala mifumo yao ya fahamu.

Hawa huamini kuwa, ‘kelele’ za wasiowapenda zinapaswa kuzimwa bila kujali wanapanda mbegu gani, kinachowatosha wao ni ‘uungu’ katika uso wa dunia. Hizo ndio akili zao.

Wamefunika historia kwamba, wakoloni hawakuondoka kwa mahaba na waafrika, kilichowasukuma kufanya hivyo ni muda.

Tukumbushane kwamba hakuna aliye salama katika mazingira yanayotawaliwa na utesaji, utekani na upotezwaji, kila mwenye nafasi anapaswa kupinga na kukemea.

Tukumbushane kuwatekwa, kuteswa na kupotezwa ni mambo tusiyoyataka na hayavumiliki. Jukumu la kuzuia haya ni la kila mmoja wetu. Wakati ni sasa.

error: Content is protected !!