Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Shuwasa yaainisha maeneo yatakayotwaliwa kwa ajili ya mradi wa AFD
Habari Mchanganyiko

Shuwasa yaainisha maeneo yatakayotwaliwa kwa ajili ya mradi wa AFD

Spread the love

 

MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) imeainisha maeneo matatu katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambayo yatatumika kujenga miundombinu ya majitaka na majisafi katika Kata za Iselemagazi, Didia na Tinde. Anaripoti Mwandishi Wetu, Shinyanga … (emdelea).

Maeneo hayo ambayo yatakuwa na jumla ya hekari 30 yanatarajia kutwaliwa baada ya kushirikisha wamiliki wakeambao watalipwa fidia kwa mujibu wa Sheria zinazoongoza utwaaji wa ardhi.

Akizungumza wakati wa kubaini maeneo hayo kwa ushirikiano wa wataalamu wa upimaji ardhi kutoka ofisi za mkoa na wilaya, Mhandisi wa Mzingira na Usafi kutoka SHUWASA, Bundala Igambwa, amesema Mamlaka hiyo imekuwa ikitoa huduma za majisafi katika maeneo hayo ambayo baada ya matumizi huzalisha majitaka kwa asilimia 80.

Amesema kutokana na hali hiyo Mamlaka kupitia mradi unaofadhiliwa na Shirika la Maendelo la Ufaransa (AFD) kwa ushirikiano na Serikali ya Tanzania, inatarajia kujenga mitambo ya kuchakata majitaka katika Kitongoji cha Mwamaguku kijiji cha Mwamakalanga utakaohudumia mji mdogo wa Iselemagazi.

Amesema pia mitambo kama hiyo ya uchakataji majitaka, itajengwa katika kitongoji cha Ipanda kijiji cha Kituli kata ya Tinde na itahudumia maeneo ya Tinde na Didia.
“Tumechagua eneo la Ipanda kwasababu lipo katikati ya Tinde na Didia hivyo itakuwa rahisi kuhudumia maeneo yote,” amesema Mhandisi Igambwa.

Amesema kazi kubwa ya mitambo hiyo ni kuchakata majitaka yanayozalishwa na kuyabadili kuwa majisafi yanayofaa kurudishwa katika mazingira bila kuwa na athari.

Kwa upande wa mji mdogo wa Didia amesema eneo hilo limekuwa na maendeleo ya makazi na kuongeza uhitaji wa huduma ya majisafi hivyo SHUWASA inatarajia kujenga miundombinu mikubwa ya majisafi katika kitongoji cha Danduhu kijiji cha Didia itakayohusisha tangi kubwa la majisafi na baadae ofisi na nyumba za watumishi.

Mhandisi Igambwa amesema zoezi la utwaaji wa maeneo hiyo litakuwa shirikishi kwa kukutana na kujadiliana na wamiliki na viongozi wa Serikali ngazi mbalimbali kwaajili ya utaratibu wa kulipa fidia kwa mujibu wa sheria.

“Lengo la kutembelea maeneo haya ni kuyabaini na kuwaonesha viongozi wa Serikali za Mitaa ili waweze kuwatambua wamiliki wake tuweze kukutana nao kwaajili ya majadiliano, uthamini na kulipa fidia, ili tutekeleze miradi hii ambayo ni kwa faida yao,” amesema Igambwa.

Akizungumzia suala hilo Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwamakalanga, James Washa, amesema amepokea suala hilo na atalifikisha kwa wamiliki wa maeneo yaliyobainishwa ili kukutana na SHUWASA kwa majadiliano.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Gardner Habash wa Clouds Fm afariki dunia

Spread the loveALIYEKUWA mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

error: Content is protected !!