Friday , 1 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Shura ya Maimamu kukata rufaa kupinga Sheikh kufungwa miaka 7
Habari Mchanganyiko

Shura ya Maimamu kukata rufaa kupinga Sheikh kufungwa miaka 7

Sheikh Ponda Issa Ponda (katikati)
Spread the love

SHURA ya Maimamu Tanzania, inakusudia kukata rufaa dhidi ya hukumu ya kwenda jela miaka saba, aliyohukumiwa Sheikh Dua Said Linyama, baada ya kukutwa na hatia  kwenye mashtaka ya ugaidi yaliyokuwa yanamkabili kwenye Mahakama Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Kusudio hilo limetangazwa hivi karibuni na Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, baada ya hukumu hiyo kutolewa tarehe 4 Desemba 2023, mahakamani hapo.

Taarifa ya Sheikh Ponda imedai kuwa, Linyama alipewa adhabu hiyo akidaiwa kukutwa na silaha (bomu), kinyume cha sheria. Alikamatwa akiwa nyumbani kwake Tegeta mkoani Dar es Salaam, tarehe 26 Agosti 2015.

“Shura ya Maimamu Tanzania, inajiandaa kukata rufaa dhidi ya hukumu ya miaka saba iliyotolewa kwa bwana Dua Saidi Linyama,” ilisema taarifa ya Sheikh Ponda.

Katika hatua nyingine, taarifa hiyo imesema mahakama iliwaacha huru washtakiwa wengine sita waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka ya ugaidi, halafu baadae Jeshi la Polisi liliwakamata tena kisha kuwaacha huru kwa masharti ya dhamana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Karafuu, Parachichi yawa fursa Morogoro

Spread the loveIMEELEZWA kuwa zao la karafuu ambalo kwa sasa linalimwa pia...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Washindi 12 NMB MastaBata na wenza wao wapaa Afrika Kusini

Spread the loveWASHINDI 12 wa kampeni ya kuhamasisha matumizi yasiyohusisha pesa taslimu...

Habari Mchanganyiko

4 wanusurika kifo ajali ya ndege Serengeti

Spread the loveWATU wanne wakiwamo abiria watatu na rubani mmoja wamenusurika kifo...

Habari Mchanganyiko

Mafua yamtesa Papa, afuta mikutano

Spread the loveKiongozi wa Kanisa katoliki duniani, Papa Francis amelazimika kufuta mkutano...

error: Content is protected !!