
Wanafunzi wa shule ya msingi, Namtumbo
IDARA ya Ukaguzi wa shule ina upungufu wa wakaguzi 341. Taarifa hiyo ilitolewa bungeni leo na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Anne Kilango wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Rita Kabati (CCM). Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).
Katika swali lake Kabati alitaka kujua mkakati wa Serikali wa kuimarisha Idara ya Uakaguzi wa Elimu nchini.
Kilango amesema hadi kufikia mwaka 2013/14 Idara ya Ukaguzi wa shule ilikuwa na idadi ya wakaguzi 1,109 na upungufu wa wakaguzi wa shule 804.
“Ili kukabiliana na upungufu wa vitendea kazi,, wizara yangu kwa kushirikiana na Mradi wa Global Partneship fo Education (GPE), itapatiwa magari 45 yatakayokabidhiwa Idara ya Ukaguzi wa shule na kusambazwa katika wilaya zisizokuwa na magari,” amesema
Amesema wizara imeongeza bajeti ya matumizi mengineyo kwa ajili ya mafuta na vilainishi katika mwaka wa fedha 2015/16.
“Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi pia iko katika hatua za awali za mchakato wa kuanzisha Wakala wa Serikali wa Udhibiti wa Ubora wa Elimu Msingi,” amesema Kilango.
Amesema chombo hicho kinatarajiwa kufanya kazi nje ya wizara na kinakusudia kuleta ufanisi katika utendaji wake wa kazi kuliko ilivyokuwa awali.
More Stories
Dirisha maombi mikopo elimu ya juu kufunguliwa Julai 15
Shule za Serikali, wasichana wang’ara matokeo kidato cha sita
Watakao kwamisha mradi wa kuboresha Elimu Sekondari kukiona