Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Shule za Serikali, wasichana wang’ara matokeo kidato cha sita
ElimuTangulizi

Shule za Serikali, wasichana wang’ara matokeo kidato cha sita

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Athuman Amasi
Spread the love

 

SHULE za Sekondari za Serikali, pamoja na watahiniwa wasichana, wameng’ara katika matokeo ya mtihani wa kidato cha sita. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamebainika leo Jumanne, tarehe 5 Julai 2022, jijini Dar es Salaam, wakati Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Athuman Amasi, akitangaza matokeo ya mtihani huo uliofanyika Mei, mwaka huu.

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na Amasi, katika shule 10 bora kitaifa, shule za Serikali ziko saba huku za binafsi zikiwa tatu.

Shule iliyoshika nafasi ya kwanza katika orodha hiyo ni Kemebos, ya mkoani Kagera ambayo inamilikiwa na mtu binafsi, wakati ya pili ikiwa ni Kisimiri iliyopo Arusha, inayomilikiwa na Serikali, huku ya tatu ikiwa ni Tabora Boys (Serikali), ya nne Tabora Girls (Serikali), ya tano Ahmes iliyoko Pwani (Binafsi) na ya sita ni Dareda iliyoko Manyara (Serikali).

Kuangalia matokeo yote ya Kidato cha Singa ingia hapa 

Shule iliyoshika nafasi ya saba ni, Nyaishozi kutoka Kagera (binafsi),ya nane Mzumbe kutoka Morogoro (Serikali), ya tisa Mkindi kutoka Tanga (Serikali), na ya kumi ni Ziba kutoka mkoani Tabora (Serikali).

Kwa upande wa watahiniwa waliofanya vizuri zaidi kitaifa katika mtihani huo kwenye masomo ya sayansi, wasichana wamekuwa kinara ambapo wako saba wote kutoka Shule ya Sekondari ya St. Mary’s Mazinde Juu, iliyoko mkoani Tanga, huku wa kiume wakiwa watatu kutoka Shule ya Tabora Boys, ya mkoani Tabora.

Katika orodha hiyo, wa kwanza ni Catherine Mwakasege, Lucy Magashi (wa pili), Muhewa Kamando (wa tatu), Minael Mgonja (wa nne), Norah Kidjout (wa tano), Jennifer Chuwa (wa sita), Pauline Mabamba (wa saba), Rachel Joachim Moshy (wa nane ) Kulwa Mbizo Elias (wa tisa) na Oscar Eliakim Marabe (wa 10).

Kwa upande wa watahiniwa 10 waliofanya vizuri katika masomo ya lugha na sanaa kitaifa, wavulana wako sita na wasichana wako wanne, ambapo wa kwanza ni Hamza Ngosse kutoka Shule ya Songea Boys, mkoani Ruvuma, wa pili Charite Chonza, kutoka Zakia Meghji ya Geita, wa tatu Zilabhela Kombwey, kutoka Kisimiri iliyoko Arusha.

Wa nne ni Mebo Mgaya, kutoka Shule ya Ahmes ya mkoani Pwani, wa tano Gilead Gwaselya, kutoka Tukuyu ya Mbeya, wa sita Albert Boniphace kutoka Kisimiri, Arusha. Wa saba Abdallah Mtawanyika kutoka Kemebos ya mkoani Kagera.

Aliyeshika nafasi ya nane ni Winfrida Sugoya, kutoka Ahmes ya mkoani Pwani , wa tisa Hassan Buruhani kutoka Musoma mkoani Mara na wa mwisho Erick Godvin Mlay, kutoka Dareda ya mkoani Manyara.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

error: Content is protected !!