June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Shule za Kata zinatoa ushindani’

Moja ya shule za kata nchini

Spread the love

OFISI ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imetoa takwimu za ufaulu katika mitihani ya kitaifa ambazo zinaonesha kati ya  watahiniwa waliofaulu kwa Daraja I-III ambao ndiyo wana sifa za kujiunga na Elimu ya Juu na mafunzo mbalimbali, walitoka Shule za Sekondari za Kata. Anaandika Dany Tinason … (endelea).

Naibu Waziri wa Tamisemi Aggrey Mwarni aliliambia bunge jana kuwa, wahitimu hao ni sawa na asilimia 88.25 na kuwa, hali hiyo inayoonyesha Shule za Sekondari za wananchi (Kata), zinatoa wanafunzi wengi zaidi kwa hali ya ushindani.

Alitoa majibu hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Ileje, Aliko Kibona (CCM) ambaye alitaka kujua kama Serikali haioni ni kutengeneza ufa na ubaguzi kwa wenye nacho na wasionacho katika masomo ya sayansi kwa shule za Kata ambazo hazina miundombinu ya kutosha kwa masomo ya sayansi.

“Je Serikali haioni ipo haja ya kurejea kwenye misingi ya Azimio la Arusha la kila mtu kupata haki sawa bila kubaguliwa kwa sababu ya kipato ili kuendelea kulinda umoja, upendo na mshikamano katika taifa?” amehoji Kibona.

Naibu Waziri amesema, Shule za Sekondari nchini zimeendelea kuimarishwa ikiwemo Sekondari za Kata.

Amesema, sifa zinazotumika kudahili wanafunzi zinazingatia hali halisi ya mahitaji kitaaluma katika kujiunga na mafunzo mbalimbal ikiwemo uuguzi ambapo utaratibu unaweka uwiano sawa kwa wanafunzi wote wenye sifa za kujiunga mafunzo ikiwemo wanafunzi wanaotoka Shule za Kata.

Amesema, serikali itakarabati na kukamilisha Shule za Sekondari 1200 za wananchi kwa kiwango cha kuwa na mindombinu yote muhimu ikiwemo maabara na awamu ya kwanza imekamilisha shule 264 ambazo zilitengewa Sh 56.3 bilioni.

Awamu ya pili itahusisha shule 528 na awamu ya tatu shule 408 kwa mwaka 2014 ambapo serikali ilitoa pia Sh. 1.1 bilioni kwa Shule za Sekondari 75 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa  vya maabara na ukarabati mdogo.

error: Content is protected !!