Monday , 27 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Shule ya Alpha yazindua mfumo wa kugundua vipaji vya watoto
Elimu

Shule ya Alpha yazindua mfumo wa kugundua vipaji vya watoto

Mratibu wa Mtaala wa ziada wa Shule ya Sekondari ya Alpha, Fulgence Kabiligi
Spread the love

 

SHULE ya Sekondari ya Alpha ya jijini Dar es Salaam imezindua mfumo wa kupima na kugundua vipaji vya watoto kidigitali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mfumo huo utahusika kupima vipaji vya watoto kijidigitali ili kuweza kusaidia watoto kuendelezwa katika vipaji vyao na kuvitumikia ipasavyo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo huo Profesa wa Sheria na mtoa mihadhara maarufu kutoka nchini Kenya, Patrick Lumumba, alisema watasambaza ujumbe huo mzuri kuwa shule za Alpha ndio zimechaguliwa kuwa kitovu anzilishi cha mfumo huo mpya ambao utakuwa na manufaa kwa vijana wa kike na wakiume wa kitanzania na Afrika pia.

Prof Lumumba alieleza kuwa kupitia mfumo huo vijana watakaotambuliwa vipaji vyao watawezeshwa ili mafanikio yao yasikwazwe bali yapewe rutuba.

“Kupitia mfumo huu mtoto atapimwa kipaji chake na kusaidiwa kukitumia vizuri. Kila mtu ana kipaji ila wengine hawajui hivyo kushindwa kuvitumia ipasavyo,”alisisitiza Prof Lumumba.

Kwa upande wake Mratibu wa Mtaala wa ziada wa shule ya Alpha, Fulgence Kabiligi, alisema hata kabla ya ujio wa mashine hiyo, shule yao ilijikita kugundua vipaji kwa kuanzisha vilabu 21 na kufundisha jinsi ya kuwa wajasiriamali.

“Hii mashine ni kwa ajili ya Watanzania wote kwani itagundua watoto wenye uwezo mkubwa, mdogo na ambao hawana watatafutiwa utaratibu.

Alisema manufaa yake inamsaidia kupima kipaji na kukijua na kuendelezwa katika shule ya kipaji husika na kusoma kwa haraka na muda mfupi ili kuweza kutumia kipaji chake.

“Mtoto anapimwa na mwanasaikolojia kujua historia yake, asili na anapendelea nini baadae anaingia kwenye mashine inachukua vina saba na wanatoa michoro ambayo inatumwa mtandaoni wanasoma na kurudisha majibu ndani ya dakika chache,”alieleza Kabaligi.

Alifafanua kuwa watakuwa na kliniki zitakazoendeleza vipaji, vyuoni na watashirikiana na shirikisho la vipaji duniani na kupima vipaji na wakigundulika watachukuliwa kwenda nje kwa lengo la kuendelezwa.

Alifafanua kuwa mashine hiyo ni kamera ya kawaida haina mionzi wala madhara kwa binadamu.

“Tutaweka uratibu wa kupima kwa watu ambao hawana uwezo tutatumia serikali za mitaa na tutatumia pia utaratibu taratibu za shirikisho la vipaji duniani na kliniki zitakuwa na gharama kidogo tutashirikiana na serikali,”alisisitiza.

Naye Afisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Abdul Maulid, alisema ikiwa watoto watapimwa kupitia mfumo huo itarahisisha kwani wapo wazazi wanawalazimisha watoto kusoma mambo ambayo hawana uwezo nayo.

Alisema wao wanatumia waalimu kugundua vipaji vya watoto kutokana na elimu walizopatiwa kwa muda mrefu.

“Tulikuwa tunajua kuwa huyu mwanafunzi anafaa kusoma sayansi, biashara au sanaa kwa kumfuatilia ufaulu wake, ila mfumo huo utaondoa shida kwa mzazi kutaka mtoto wake kuwa kama yeye atafata kipaji chake,”alisisitiza.

1 Comment

  • @THINK/Dedication/Remember”@ EMPLOY/US THEM ALL – ALL TANZANIAN HAS JOB TO DO

    In 2021, the unemployment rate in Tanzania remained nearly unchanged at around 2.74 percent. With a decline of 0.04 percentage points, there is no significant change to 2020. Over the observed period, the unemployment rate has been subject to fluctuation.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari Mchanganyiko

Rubani mtarajiwa Tusiime awashangaza wazazi

Spread the loveWAZAZI walioshiriki siku ya taaluma na maonyesho ya shule ya...

BiasharaElimu

Benki ya Exim yazindua huduma ya ‘Exim Smart Shule’

Spread the love  KATIKA juhudi za kuboresha teknolojia za kidijitali katika sekta...

Elimu

Waziri SMZ akoshwa na kazi za Global Education Link

Spread the loveSERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar SMZ imesema itaendesha msako na kuzifutia...

ElimuHabari za Siasa

Serikali kuongeza wanufaika mikopo ya elimu ya juu

Spread the loveSERIKALI imesema itaongeza idadi ya wanufaika wa mikopo ya elimu...

error: Content is protected !!