Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Shule sasa kuvuna maji ya mvua
Habari za Siasa

Shule sasa kuvuna maji ya mvua

Spread the love

 

WIZARA ya Maji kwa kushirikiana na Tawala za Miko ana Serikali za Mitaa (TAMISEMI), watakutana kuweka mkakati wa kuhamasisha shule kujenga gata za maji na matanki ili kuvuna maji ya mvua. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 15 Aprili 2021, na Jumaa Aweso, Waziri wa Maji akijibu swali la Zainabu Katimba, Mbunge Viti Maalum (CCM).

Katika swali lake, Zainabu ameuliza “Kijiographia Tanzania ipo kwenye ukanda wenye mvua za kutosha, Je serikali imejizatiti vipi kuhamasisha zoezi la uvunaji wa maji ya mvua kwa matumizi ya wananchi?”

Waziri Aweso amesema, ni kweli Tanzania ipo kwenye ukanda wenye mvua za kutosha hivyo, ujenzi wa miundombinu ya kuvuna maji ya mvua ni muhimu kwa kuwa, itawezesha kuwa na maji ya uhakika kwa kipindi chote cha mwaka bila kujali hali ya hewa.

Na kwamba, miundombinu hiyo ni muhimu kwa kuwa itawezesha kudhibiti mafuriko na hivyo kuokoa miundombinu, ikiwemo ya huduma za maji pamoja na mali na maisha ya wananchi.

Zainab Katimba, Mbunge wa Viti Maalum Kigoma

“Serikali inaendelea na mpango wa ujenzi na ukarabati wa mabwawa kwa kila wilaya hususan katika wilaya kame. Kwa mwaka wa fedha 2020/21, wizara imekamilisha ukarabati wa bwawa la Mwadila lililopo Wilaya ya Maswa, Mkoa wa Simiyu,” amesema.

Waziri huyo amesema, usanifu kwa ajili ya kukarabati mabwawa matatu (3) ya Itobo liliopo Wilaya ya Nzega, Engukument lililopo Wilaya ya Monduli na Horohoro lililopo Wilaya ya Mkinga, na usanifu kwa ajili ya ujenzi wa mabwawa mawili ya Muko na Chiwanda yaliyopo Wilaya ya Momba umeendelea.

“Vilevile, usanifu wa Malambo ya kunyweshwea mifugo (Charco dams) sita umekamilika katika mwambao wa barabara kuu ya Dodoma – Babati ikihusiha Wilaya za Bahi, malambo mawili na Chemba malambo manne.

“Vilevile, serikali inaendelea na mpango wa kujenga mabwawa ya kimkakati ya Kidunda (Mto Ruvu), Farkwa (katika Mto Bubu) na Ndembera/Lugoda (katika mto Ndembera),” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

error: Content is protected !!