October 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Shujaa wa kikapu: Kobe Bryant, hatuko naye tena

Spread the love

NI majonzi. Ni simamizi. Ni vilio kote duniani, kufuatia kifo cha ghafla cha nyota wa mpira wa kipaku nchini Marekani, Kobe Bryant. Mwanamichezo huyo mashuhuri ulimwenguni, amekutwa na mauti, kufuatia kuanguka kwa helkopta aliyokuwa anasafiria, katika eneo la Calabasas, jimboni California, nchini Marekani. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Katika ajali hiyo, Bryant alikuwa na binti yake Gianna (13) na watu wengine saba. Bingwa huyo wa NBA mara tano mefariki dunia akiwa na miaka 41. Alikuwa akisafiri na ndege binafsi – Sikorsky S-76B – aina ya helkopta, ambayo ilianguka na kuwaka moto.

Mashuhuda wa ajali hiyo, wamenukuliwa na shirika la utangazaji la BBC wakisema, ndege hiyo ilianguka nje kidogo ya mji wa Las Virgenes majira ya asubuhi wa saa za Marekani. Hakuna aliyenusurika.

Gavin Masak, alikuwa anaishi karibu na eneo ambalo ajali hiyo ilitokea na alikimbia kituo cha CBS News, kwamba alisikia sauti kubwa kama bomu limelipuka.

“Lakini ilisikika kama sauti ya ndege au helkopta, ilikuwa sauti kubwa sana. Nilinigia ndani na kumtaarifu baba yangu nilichokishuhudia. Nilivyotoka nikaona moshi mweusi ukitokea mlimani, ulikuwa mweusi au kama kijivu,” ameeleza Masak.

Naye shahuda mwingine alisema, alisikia injini ikiwa inashida hata kabla ndege haijafika chini.

Polisi wameonyesha picha za ajali hiyo zikionyesha gari la zima moto na moshi ukivuka kutoka milimani.

Kufuatia ajali hiyo, mashabiki wa mpira wa vikapu wamekuwa wakikusanyika katika eneo lililotokea ajali, huku salamu za rambirambi zikimiminika kutoka kwa watu maarufu ulimwenguni na wachezaji wenzake nyota huyo, kuonyesha mshtuko wa kifo cha Bryant.

Aidha, viwanja vyote vya mpira wa vikapu nchini Marekani, vilitenga muda wa kuwa kimya kwa heshima ya shujaa huyo.

Miongoni mwa waliotoa salamu za karibuni kabisa, ni rais mstaafu wa Marekani Barack Obama na rais wa sasa, Donald Trump.”

Akimuelezea Bryant, Rais Obama alisema, mwanamichezo huyo alikuwa bingwa na aliyeonesha umahiri katika kipaji chake.

Naye Rais Trump anasema, “…hii ni habari ya kuhuzunisha sana,” huku  Shaquille O’Neal, ambaye alicheza na Bryant huko Lakers kati ya mwaka 1996 na 2004, akisema “sina neno la kutokana na maumivu niliyonayo.”

Akiandika katika mtandao wa Instagram wakiwa katika picha ya pamoja na jezi zao za Lakers alisema, “ninakupenda na utakumbukwa.”

Deron Williams, alikuwa mshindi wa medali ya dhahabu ya Olympiki akiwa na Bryant, aliishiwa maneno. Alimuelezea Bryant kuwa mchezaji bingwa aliyewahi kucheza naye.

Usain Bolt ambaye ana medali nane za dhahabu za olimpiki alisema kuwa haamini taarifa hizi.

Mwanamuziki Kanye West aliandika katika mtandao wa twitter kuwa Bryant aliishi maisha ambayo yaliwavutia wengi.

Bryant atakumbukwa katika tuzo za Grammy (Gat the Grammy Awards), ambazo zilikuwa zikitolewa katika uwanja wa Los Angeles Lakers, eneo ambalo alikuwa akichezea kipindi chote.

“Tumechanganyikiwa na tuna uzuni sana kwa sasa,” alisema mtangazaji wa Grammys Alicia Keys.

“Kwa sababu mapema leo katika mji wa Los Angeles, Marekani na duniani kwa ujumla tumepoteza shujaa.”

Kobe Bryant enzi za uhai wake akiwa uwanjani

NBA ilitoa tamko linalosema, imesikitishwa sana na ajali iliyosababisha kifo cha Kobe Bryant na binti yake, Gianna.

Kwa misimu 20, Kobe alionyesha kile ambacho kinawezekana kwa mtu ambaye ana kipaji na nia ya ushindi.

Bryant alicheza mpira wa kikapu kwa 20-katika viwanja vya Los Angeles Lakers. Aliacha kucheza mchezo huo Aprili 2016.

Mafanikio yake ni pamoja na kuwa mchezaji bingwa wa NBA kwa mwaka 2008, mara mbili aliibuka kuwa bora zaidi ya wengine. Alikuwa pia mfungaji bora wa NBA pamoja na bingwa mara mbili wa mashindano ya Olympiki.

Aliwahi kupata pointi 81 dhidi ya wachezaji wa Toronto Raptors mwaka 2006, katika historia ya michezo ya NBA.

Mashabiki wa Kobe Bryant wakiwa eneo la tukio ambapo mkongwe huyo wa mpira wa kikapu alipopoteza maisha kwa ajali ya helkopta

Bryant alishinda tuzo za Oscar kama mchezaji wa filamu fupi mwaka 2018 filamu hilo ilikuwa ‘Dear Basketball’, filamu ya dakika tano iliyoangazia barua moja ya michezo aliyoandika mwaka 2015.

Bryant na mke wake, Vanessa, walikuwa na watoto wengine wakike watatu ambao ni Natalia, Bianca na Capri.

Hata hivyo, mwaka 2003, Bryant aliwahi kushitakiwa mahakamani kwa makossa ya unyanyasaji wa kingono na binti mwenye miaka 19, aliyekuwa akifanya kazi katika mgahawa wa Coloradot.

Lakini mwenyewe alikanusha madai hayo, na kusema kuwa walikuwa na mahusiano ya kimapenzi na walikubaliana. Kesi hiyo ilifutwa baada ya mtu aliyemshtaki kukataa kutoa ushahidi mahakamani.

Ingawa baadaye aliomba radhi kwa kitendo kile na kuongeza kuwa msichana aliyekuwa naye hakuwa na mtazamo sawa na wake, wakati walipokuwa kwenye mahusiano yao.

error: Content is protected !!