Sunday , 29 January 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko ‘Shughuli za kibinadamu, kilimo zinaathiri hifadhi’
Habari Mchanganyiko

‘Shughuli za kibinadamu, kilimo zinaathiri hifadhi’

Hifadhi ya Arusha
Spread the love

 

MENEJA Ushirikishwaji wa Sekta Binafsi wa Mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili Dk. Elikana Kalumanga amesema shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo ni moja ya vitu vinavyoathiri maeneo yanayounganisha hifadhi mbalimbali nchini (shoroba) zinatumiwa na wanyamapori. Anaripoti Selemani Msuya, Pwani … (endelea).

Dk. Kalumanga amesema hayo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari za mazingira kuhusiana na mradi huo yanayoratibiwa na Chama cha Waandishi wa Habari wa Mazingira Tanzania (JET) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID).

Alisema shoroba zimekuwa zikiathiriwa na shughuli za kibinadamu na kuhatarisha uwepo wa maeneo hayo na maisha ya wanyama hao kwa ujumla, hivyo ni jukumu la kila mwananchi kushiriki kuzuia hali hiyo.

“Hali za shoroba nyingi si nzuri kwani kwa mujibu wa takwimu za serikali zipo baadhi, zimepotea kabisa kutokana na shughuli hizo za wananchi zinazofanywa kila siku, hasa kilimo, kuna haja ya kuendelea kuwaelimisha wananchi,” alisema.

Meneja huyo amewataka waandishi wa habari kuwa mstari wa mbele kuibua na kuelimisha jamii juu ya athari zitokanazo na shughuli hizo za kibinadamu ndani ya shoroba pamoja na faida za kiuchumi zinazopatikana.

Dk. Kalumanga amesema kwenye shoroba wananchi wanapata vitu vingi kama kuni na dawa, hivyo zinapaswa kutunzwa na kuendelezwa.

“Shoroba ya Laja inayotoka hifadhi ya Taifa ya Manyara kuelekea eneo la hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, kule utawakuta hawa ndugu zetu wa Wahadzabe ambao wanatengemea maeneo hayo kupata rasilimali zao za kila siku ikiwemo chakula na makazi, ili ziweze kuendelea ni vema shughuli za kibinadamu kama kilimo zisitishwe,” alisema..

Alisema waandishi wakitumia kalamu zao vizuri shoroba hizo zitaweza kuongeza idadi kubwa ya wanyamapori ambao watavutia watalii na kuchochea ongezeko la uchumi wa nchi na wananchi.

Meneja huyo alisema hata Sheria ya Wanyamapori ya 2009, inaweka wazi kuwa maeneo ya shoroba ambayo yanatumiwa na wanyama hao yasitumike kwa shughuli za kijamii kama kilimo na nyinginezo.

Alisema iwapo Serikali na wananchi wataweka mkazo katika kuzilinda shoroba, mapori ya akiba, hifadhi za taifa, misitu ya asili na mingine ni wazi kuiwa wanyamapori watakuwa salama katika makazi na njia zao.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa JET, John Chikomo alisema kupitia Mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili, wanaamini jamii itaweza kubadilika katika kufuata sheria zilizopo, ili kuepuka kuingilia maeneo ya wanyamapori.

Alisema iwapo kila mwandishi ambaye ameshiriki mafunzo hayo atazingatia misingi ya taaluma hiyo katika kutoa elimu kwa jamii ni wazi changamoto ambazo wanyamapori wanakutana nazo kwa maeneo yao kuingiliwa zitapata ufumbuzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Huawei Tanzania yatajwa miongoni mwa waajiri bora kimataifa

Spread the loveKAMPUNI ya Huawei Tanzania imetajwa kuwa mwajiri bora nchini na...

Habari Mchanganyiko

Waziri wa uchumi wa Finland atua nchini, kuteta na mawaziri 7

Spread the loveWAZIRI wa Masuala ya Uchumi wa Finland, Mika Tapani Lintilä...

Habari Mchanganyiko

Asimilia 79 wafeli somo la hesabu matokeo kidato cha nne

Spread the loveWATAHINIWA wa shule 415,844 sawa na asilimia 79.92 ya watahiniwa...

Habari Mchanganyiko

NECTA yafuta matokeo ya watahiniwa 333 kwa kuandika matusi, kudanganya, 286 yazuiwa

Spread the loveBARAZA la Mitihani la Tanzania (Necta) leo Jumapili limetangaza kuyafuta...

error: Content is protected !!