KATIBU wa Bunge la Tanzania, Nenelwa Mwihambi ametangaza kusitisha shughuli zote za Bunge ikiwemo kamati za Bunge zilizokuwa zikutane kuanzia tarehe 10 Januari 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Kamati hizo, zilikuwa zinakutana kwa ajili ya maandalizi ya mkutano wa Bunge utakaoanza tarehe 1 Februari 2022.
Taarifa ya Nenelwa aliyoitoa leo asubuhi Ijumaa tarehe 7 Januari 2022, imesema amechukua uamuzi huo baada ya aliyekuwa spika, Job Ndugai kujiuzulu nafasi hiyo jana Alhamisi.
Amesema kwa mujibu wa Ibara ya 84(1) ya Katiba ya Tanzania yam waka 1997, Spika ndiye kiongozi wa Bunge na ndiye msimamizi wa shughuli zote za Bunge.
Aidha, Ibara ya 84(8) inaelekeza kwamba kiti cha spika kinapokuwa wazi hakuna shughuli yoyote itakayotekelezwa katika Bunge isipokuwa uchaguzi wa Spika.
Amewataka wabunge kuwasili Dodoma tarehe 31 Januari 2021.
Kwa maana hiyo, mara ya Bunge kukutana tarehe 1 Februari 2021, shughuli ya kwanza itakuwa kumchagua spika.
Yes