Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa ‘Shubiri’ inayomsubiri ‘Rais’ Ndayishimiye
Kimataifa

‘Shubiri’ inayomsubiri ‘Rais’ Ndayishimiye

Evariste Ndayishimiye, Rais wa Burundi
Spread the love

JENERALI Evariste Ndayishimiye, rais mteule wa Burundi, anaapishwa leo kuongoza taifa hilo kwa miaka saba, anachukua nafasi ya Pierre Nkurunziza ambaye alifariki dunia tarehe 8 Juni 2020. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Ndayishimiye alitarajiwa kuapishwa Agosti 2020 kwa mujibu wa ratiba ya Tume ya Uchaguzi ya Burundi, tariba hiyo imebadilishwa kutokana na Nkurunziza kufariki dunia, hivyo kuhofia taifa kutokuwa na amiri jeshi mkuu kwa muda mrefu.

Rais huyo mpya anaichukua Burundi wakati ambao ina ‘matobo’ mengi ikiwemo uhusiano wake na nchi jirani, utulivu wa kisiasa ndani ya nchini na ukabila. Nkurunziza ameiacha Burundi ikiwa si salama, jambo kubwa alilotuhumiwa katika utawala wake ni kuuawa wale waliokuwa wakimpinga.

Rais mteule Ndayishimiye kupitia chama chake – chama tawala – CNDD-FDD, alipata ushindi wa asilimia 68.72 dhidi ya hasimu wake mkuu Agathon Rwasa wa chama cha CNL aliyepata asilimia 24.19.

Kulipa fadhila

Ndayishimiye anajua kabisa, kwamba hakuwa chaguo la Nkurunziza, uteuzi wake ulisukumwa na majenerali wengine ndani ya CNDD-FDD. Chaguo la Nkurunziza lililofeli lilikuwa Pascal Nyabenda ambaye alikuwa Spika wa Bunge.

Ndayishimiye anaongoza taifa huku akitakiwa kutimiza matakwa ya watu inafsi waliomsukuma kufikia kiti hicho, waliompigania wanajua nini wanataka na Ndayishimiye naye anajua nini wanataka. Kukiuka matakwa hayo kunaweza kumpa wakati mgumu kwenye utawlaa wake hasa kuzingatia historia hasi ya taifa hilo.

Ndayishimiye anaweza kulazimika kupindisha utekelezaji wa sera zake ili ‘kulipa fadhila’ kwawaliombeba na kumpachika kwenye kiti hicho cya urais.

Uhasama

Ndayishimiye anayo changamoto kubwa ya kumaliza uhasama kati ya taifa lake na Rwanda. Mara kwa mara mtangulizi wake (Nkurunziza) na serikali ya Kigali, Rwanda walikuwa wakiingia kwenye mvutano wakituhumiana uasi.

Tuhuma za mara kwa mara ziliharibu kabisa uhusiano wa Rwanda na Burundi. Rwanda iliituhumu Burundi kuhatarisha usalama wake huku Burundi ikipeleka tuhuma hizo hizo kwa Rwanda. Nxhi hizo mbili ilikuwa nchi moja lakini zilitenganishwa na wakoloni.

Tangu kukatika kwa uhusiano wa Rwanda na Burundi mwaka 2015, kwa mara ya kwanza Paul Kagame, Rais wa Rwanda alituma salamu za rambirambi baada ya kifo cha Nkurunziza.

Ukabila

Mauaji ya kikabila ya mara kwa mara Burundi, yamesababisha kuzalisha wakimbizi kwa muda mrefu. Burundi kwa miaka mingi, imekuwa ikikimbiwa na wakazi wake waliohamia nchi za jirani ikiwemo Tanzania na Rwanda ili kukwepa kuuawa.

Rekodi zinaonesha, zaidi ya raia 350,000 wanaishi ukimbizini katika nchi jirani huku wengine 110,000 wakiwa wakimbizi wa ndani ya nchi.

Wakimbizi wa Burundi watasubiri kuona iwapo Ndayishimiye ataweka mazingira salama yatakayowawezesha kurejea na kuishi tena nchini mwao.

Uchumi

Uchumi wa Burundi kuanzia mwaka 2015, umekuwa ukizorota. Viwango vya umaskini vimepanda hadi kufikia asilimia 74. Burundi kwa sasa ni nchi ya tatu masikini zaidi duniani.

Ndayishimiye atatakiwa kushughulikia viwango vya juu vya ukosefu wa ajira na umasikini mkubwa. Wahisani wengi wa kimataifa wamesitisha misaada wao wa Burundi baada ya uchaguzi wa 2015, jambo lililosababisha uhaba mkubwa wa fedha za kigeni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaKimataifa

Faye aahidi kuongoza kwa unyenyekevu, wagombea wenzie wakubali yaishe

Spread the loveMgombea wa upinzani Senegal, Bassirou Diomaye Faye anajiandaa kuwa rais...

Habari MchanganyikoKimataifa

Wanafunzi 130 waliokuwa wametekwa nyara waokolewa

Spread the loveZaidi ya wanafunzi 130 wa shule ya msingi LEA na...

Habari MchanganyikoKimataifa

Mgombea upinzani aongoza uchaguzi wa Rais Senegal

Spread the loveMgombea wa upinzani nchini Senegal, Bassirou Diomaye Faye ameonekana kuongoza...

error: Content is protected !!