June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Shivji: Msitafute madaraka bila malengo

Mhadhiri mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Issa Shivji

Spread the love

MHADHIRI mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Issa Shivji, amevionya vyama vya siasa vinavyotafuta madaraka bila kujua lengo mahususi ya wanaotaka kuwaongoza. Anaandika Pendo Omary … (endelea). 

Prof. Shivji ametoa onyo hilo wakati akizungumzia nafasi ya vyama vya siasa na wanasiasa wakati wa harakati za ukombozi wa Bara la Afrika, katika maadhimisho ya wiki yaliyozinduliwa jijini Dar es Salaam.

Shivji amesema ipo tofauti kati ya vyama vya ukombozi na vyama vya siasa. “Chama cha ukombozi lengo lake ni kukomboa nchi wakati chama cha siasa lengo lake ni kuingia madarakani na kushika dola,”amesema Shivji.

Amesema kuwa chama cha ukombozi kinakusanya nguvu za umma bila kujali tofauti zao wakati chama cha siasa kinatumia wafuasi wake na mifarakano katika jamii kama nyenzo ya kujipatia wafuasi wengi zaidi.

Aidha, Shivji ametaja tofauti nyingine kuwa ni chama cha ukombozi huongoza wakati wakuu wa vyama vya siasa hushawishi au kuchochea; Vyama vya ukombozi bado vinaamini uwepo wa ubeberu, hivyo vinahitaji viongozi bora wakati vyama vya siasa haviamini uwepo wa ubeberu.

“Kiongozi bora ni yule anayemwezesha mwananchi kujitawala. Vyama vya siasa vinavyotafuta madaraka bila kujua malengo ya kujikomboa vitabaki kuwaitwa vibaraka wa wakoloni,” ameeleza Shivji.

Akizungumza kwa niamba ya mgeni rasmi, Bernard Membe- Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika uzinduzi huo, Mahadhi Juma Maalim, Naibu Waziri wa wizara hiyo, amesema upo umuhimu wa kuhifadhi kumbukumbu za wapigania uhuru wa Bara la Afrika.

“Kama utunzaji wa kumbukumbu za wapigania uhuru zitatunzwa vizuri itasaidia kuelimisha umma kuhusu harakati za ukombozi wa bara la Afrika,”amesema Maalim.

Naye Filiberto Ceriani Sebregondi, Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania na Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC), amesema Tanzania ilikuwa mstari wa mbele katika jitihada za ukombozi wa bara la Afrika.

“Katika jitihada hizi, ilitoa makazi kwa wapigania uhuru wa kiafrika katika miaka ya 60. EU ni mshirika katika mradi wa TAHAP ambapo tunatoa mchango wa Sh. 2 bilioni katika kuwezesha mradi huu,” amesema Sebregondi.

 

error: Content is protected !!