September 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Shitaka hili limemtibua Lema

Godbless Lema, Mbunge wa Arusha Mjini (katikati) akizungumza na waandishi muda mchache baada ya kutoka mahakamani mjini Singida

Spread the love

SHITAKA la kusababisha kuibua taharuki linalomkabili Godbless Lema, Mbunge wa Arusha Mjini, limemtibua. Anaripoti Mwandishi Wetu, Singida … (endelea).

Nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida, leo tarehe 25 Machi 2020, Lema ameonesha kushangazwa na shitaka hilo huku akihoji ‘nani aliyetaharuki?”

Lema amepandishwa kizimbani kwenye mahakama hiyo akikabiliwa na jumla ya mashtaka 15 likiwemo la kuibua taharuki kwa jamii.

Amepandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka hayo na mawakili upande wa Jamhuri, mbele ya Consolata Singano, Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo.

Mawakili hao wa serikali ni Michael Ng’hoboko, Monica Mbogo, Caren Malando na Rose Cholongola.

Katika mashtaka hayo, Lema anadaiwa kusababisha taharuki kwa jamii, kupotosha jamii. Anadaiwa kufanya makosa hayo tarehe 29 Februari 2020, akiwa mjini Manyoni mkoani Singida, kwenye mazishi ya kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Pia, anadaiwa kusambaza taarifa za uongo katika mitandao ya kijamii, zenye nia ya kupotosha jamii, kuhusu mauaji ya watu 14.

Hata hivyo, Lema ameachiwa kwa dhamana baada ya kukana mashtaka yote. Kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 15 Aprili 2020.

error: Content is protected !!