Spread the love

 

MSAFARA mdogo wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu , International Geneve Comitee [ICRC] wa magari matatu, umeondoka kutoka Zaporiahzhia , kuelekea Mariupol kwa lengo la kujaribu kuwasaidia Raia kutoka mji uliozingirwa na Warusi.

Hata hivyo Timu hiyo ilipokea dhamana za Usalama uliohitajika mapema.

Aidha wanataka kufanya operesheni hiyo , kwa siku moja wakitarajia kupata mabasi kwa ajili ya kuwahamisha raia, kutoka maeneo yaliyozingirwa na , kuwapeleka kando ya barabara.

Msaidizi wa Meya wa Moriupol Petro Andryuschenko amesema kwamba , Jiji la kusini mwa Ukraine limezingirwa na kufungwa hakuna anayejaribu kuingia au kutoka ‘’ hatari sana ‘’kwa yeyote atakayejaribu kuingia , kutoka Shirika la Habari la Reuters limeripoti.

Petro Andryschenk amesema kwamba vikosi vya Urusi , vimekuwa vikizua vifaa vya Kibinadamu kuwafikia wakazi walionaswa , hata hivyo ukanda wa kutoa misaada uliopangwa bado haujafunguliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *