Tuesday , 16 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Shirika la Meli Zanzibar lakutwa na madeni hewa Sh. 2.9 Bil.
Habari za SiasaTangulizi

Shirika la Meli Zanzibar lakutwa na madeni hewa Sh. 2.9 Bil.

Kaimu CAG Zanzibar, Dk. Othman Abbas Ali
Spread the love

 

MKAGUZI na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Visiwani Zanzibar, amegudua kuwapo kwa madeni hewa yenye thamani ya Sh. 2.9 bilioni, kwenye Shirika la Meli Zanzibar. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo ilitolewa jana tarehe 23 Mei 2021, na Kaimu CAG Zanzibar, Dk. Othman Abbas Ali, wakati akiwasilisha ripoti yake kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

Dk. Othman alitoa kauli hiyo, wakati akiwasilisha ripoti yake ya mwaka ya kazi, kwa Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi, Ikulu mjini Unguja.

Alisema, madeni hayo ya Shirika la Meli Zanzibar, hayawezi kulipika kwa kuwa hayana uhalali wowote kisheria.

“Jumla ya madeni yenye thamani ya Sh. 13.2 bilioni yaliyokaguliwa, kati yake Sh. 2.9 bilioni, hayawezi kulipika kwa kuwa hayakuweza kuthibitishwa uhalali wake,” ameeleza Kaimu CAG huyo na kuongeza, “uwepo wa deni hilo. Ndani ya shirika la Meli, ni ufujaji wa rasimali za umma.”

Kaimu CAG huyo alisema, “Shrika la Meli wamewasilisha nyaraka zinazoonysha kuna deni la kiwango hicho, lakini katika ukaguzi wangu niliofanya, nimebaini kuwa deni hilo halina uhalali wowote wa kulipwa.”

Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar

Mbali na madeni hayo hewa, Dk. Othman alisema, alishindwa kuthibitisha madeni yenye thamani ya dola za Marekani 99,258, zinalodaiwa shirika hilo na kampuni ya Green Ireland Shipping Service, kwa ajili ya matengenezo ya Meli ya Mv Maendeleo, iliyoko Mombasa nchini Kenya.

“Ukaguzi umebaini deni hilo limekosa usimamizi mzuri wa uangalizi wa gharama, zinazohalalisha uwepo wake. Meli yetu tumeipeleka Kenya kwa ajili ya matengenezo, kinachofanyakika pale ni kupokea invoice na kuthibitisha, ukaguzi wangu umeshindwa kuthibitisha uhalali wa deni hilo,” alieleza Dk. Othman.

CAG aliwasilisha ripoti yake ya kila mwaka kwa Rais Dk. Mwinyi juzi Jumapili, ambapo mara baada ya kuipokea kiongozi huyo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar alisema, yaliyomo kwenye ripoti hiyo, “yamenihuzunisha sana.”

Dk. Mwinyi alisema, ufisadi na matumizi mabaya yaliyogundulika na CAG yanathibitisha kuwa waliopewa nafasi ya kuwa viongozi wa umma, hutumia madaraka yao kujinufaisha binafsi.

Alisema, ripoti imeonyesha kuwapo kwa upotevu mkuwa wa fedha za serikali katika makusanyo na kwamba taasisi zilizopewa jukumu la kukusanya fedha zimeshindwa kufanya kazi hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za Siasa

Rais Samia amfariji mjane wa Musa Abdulrahman

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne amempa pole Mwanakheri Mussa...

Habari za Siasa

Nape: Wanasiasa, wanahabari, wafanyabiashara mteteeni Samia

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,...

Habari za Siasa

CAG: TAWA imegawa vibali vya uwindaji bila idhini ya waziri

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!