Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Shirika la Kimataifa laingilia kati kukamatwa kwa Zitto
Habari za SiasaTangulizi

Shirika la Kimataifa laingilia kati kukamatwa kwa Zitto

Spread the love

SHIRIKA la kimataifa la kutetea haki za binadamu, Amnesty International limeitaka Jeshi la Polisi kumpa dhamana au kumfikisha mahakamani, Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe anayesota rumande tangu juzi tarehe 31 Oktoba 2018. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Zitto anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam baada ya kukamatwa akiwa nyumbani kwake maeneo ya Masaki, akidaiwa kutoa taarifa za uongo kuhusu mauaji ya baadhi ya askari polisi na wananchi katika kijiji cha Mpeta wilayani Uvinza mkoa wa Kigoma.

Amnesty limetoa wito huo kupitia akaunti yake ya Twitter, ambapo limeitaka vyombo vya dola kumfungulia mashtaka mahakamani Zitto au kumuacha huru mara moja.

Wakati akizungumza na wabahari katika ofisi za ACT zilizoko Kijitonyama jijini Dar es Salaam tarehe 28 Oktoba 2018, Zitto alidai kuwa wananchi zaidi ya 100 wamepoteza maisha katika vurugu zilizoibuka kutokana na mgogoro wa ardhi wilayani Uvinza, taarifa iliyopingwa vikali na Jeshi la Polisi mkoani Kigoma.

Kabla ya Zitto kukamatwa na Polisi, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma, Martin Ottieno alimtaka Zitto kuwasilisha vielelezo vya madai yake kuwa yametokea mauaji ya watu 100 mkoani humo, ikiwemo makaburi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaTangulizi

Mapya yaibuka wamasai waliohamishwa Ngorongoro kwenda Msomera

Spread the loveMAPYA yameibuka kuhusu zoezi la Serikali kuwahamisha kwa hiari wamasai...

Habari MchanganyikoTangulizi

Baba aomba msaada kuzika miili ya familia yake iliyofunga bila kula kuonana na Mungu

Spread the loveWAKATI Mamlaka nchini Kenya, ikiendelea kukabidhi miili ya watu waliofariki...

Habari za Siasa

Rais Samia ampongeza mpinzani aliyeshinda urais Senegal

Spread the loveRAIS wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amempongeza mwanasiasa wa...

error: Content is protected !!