December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Shilingi ya Tanzania yaporomoka

Noti za Elfu Kumi

Spread the love

SHILINGI ya Tanzania kwa kipindi kuanzia Julai hadi Novemba 2018 iliporomoka ambapo Dola ya Marekani ilibadilishwa kwa wastani wa Sh. 2,276 ikilinganishwa na Sh. 2,235 katika kipindi cha Julai hadi Novemba mwaka 2017. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Akieleza kuhusu mwenendo wa shilingi ya Tanzania, George Simbachawene, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti amesema, hali hiyo inaonesha shilingi ilipungua thamani dhidi ya Dola ya Marekani kwa asilimia 1.8.

Kamati hiyo imetoa angalizo kwa serikali kuongeza jitihada ya mauzo ya bidhaa na huduma nje.

Licha ya hayo kamati inashauri viwanda vizalishe zaidi bidhaa ambazo zinaagizwa nje kwa wingi kwa kiwa hatua hizi zitasaidia kupunguza nakisi ya urari wa biashara na hivyo kuongeza upatikanaji wa fedha za kigeni na kuongeza thamani ya shilingi.

Mwenyekiti huyo amesema, serikali kwa sasa imelazimika kujielekeza zaidi kukopa mikopo yenye masharti ya kibiashara kuliko yenye mashatyi nafuu kama swali.

Na kwamba, kutokana na ugumu wa upatikanaji wa mikopo hiyo kamati bado inaona mikopo yenye mashari ya kibiashara ina riba kubwa na hivyo kuwepo kwa mzigo mkubwa wa ugharamiaji wa mikopo kupitia mapato ya ndani.

error: Content is protected !!