June 16, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Shiekh wa Mkoa atimuliwa kwa JPM

Spread the love

SHEKH Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Hassan Fereji, amezuiliwa kuingia meza kuu wakati wa mkutano wa Rais John Maguguli, anaandika Moses Mseti.

Shekh huyo ambaye aliwasili katika mkutano huo saa 15 : 34 mchana, alikuwa ameongozana na baadhi ya viongozi wa madhehebu mbalimbali Mkoa wa Mwanza kuingia katika mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya furahisha mkoani humo.

Fereje baada ya kufika katika sehemu ya kuingilia jukwaani, alikumbana na kizingiti cha Polisi pamoja na makachelo ambao walidai kuwa Shekh huyo amechelewa hivyo hapaswi kuingia.

Hata hivyo, baada ya viongozi wa CCM mkoani hapa kuona Shekh huyo amezuiliwa kuingia katika mkutano huo, walikwenda kumuomba kiongozi wa usalama wa Taifa ili kuondoa aibu hiyo lakini juhudi hizo zilikwama.

Kutokana na hali hiyo, Shekh Fereji, alilazimika kukaa pembeni ya geti la kuingia katika jukwaani, huku mazungumzo yakiendelea kufanyika namna ya kuweza kumruhusu kuingia na kwenda kukaa jukwaa kuu.

Pamoja na juhudi za viongozi hao wa CCM, za kumuomba kiongozi wa makachero hao, pia na kachero huyo alikataa kuruhusu Shekh huyo kuingia, kitendo ambacho kilisababisha Shekh huyo kurudi na kwenda kukaa kusikofahamika.

Makachero hao ambao walisikika wakisema kuwa, ” rais (John Maguguli) kashaingia kwa nini huyo Shekh (Mussa Fereji) haendi na muda’?

Mfuasi Ukuta atupwa sero

Kijana mmoja ambaye anadaiwa kuwa ni mfuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye hafahamiki jina lake, leo amekumbana na virungu vya polisi baada ya kutaka kulazimisha kuingia sehemu ambako Rais Magufuli alipokuwa amekaa.

Hata hivyo, sababu za kijana huyo anayekadiriwa kuwa na miaka 20- 25, kutaka kwenda jukwaa kuu ambako rais na viongozi wengine wakiwemo wabunge na mawaziri walikokuwa wamekaa hazikufahamika.

Polisi baada ya kuona kijana huyo wakiwa katika mvutano na vijana wa CCM, walifika na kumpiga kisha kumpandisha kwenye karandiga la Polisi na kumpelekwa kwenye Kituo cha Polisi Kirumba kilichopo Wilaya ya Ilemela mkoani humo.

error: Content is protected !!