October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Shibuda apitishwa kugombea urais Tanzania

Juma Ali Khatib, ametauliwa kuwa mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha Tadea

Spread the love

KATIBU Mkuu wa Chama cha ADA-Tadea, John Shibuda amepitishwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho, kugombea urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Pia, Juma Ali Khatib ambaye ni waziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar asiyekuwa na wizara maalum amepitishwa na wajumbe hao kugombea Urais wa Zanzibar huku Hassan Karonel Kijogoo atakuwa mgombea mwenza wa Urais wa Tanzania.

Akizungumza katika mkutano mkuu uliofanyika leo Jumanne tarehe 28 Julai 2020 jijini Dar es Salaam, Katibu wa Oganaizesheni ya uchaguzi wa chama hicho, Zuberi Hamis amesema, wagombea nafasi ya urais wa Tanania walikuwa wawili, Shibuda na na Mastadia Hilali Munika na upande wa Zanzibar alikuwa mmoja Khatib.

Amesema wanachama waliopiga kura walikuwa 130 kati ya hizo, Shibuda amepata kura 120 na Mastadia akiambulia kura 10.

John Shibuda, M/kiti baraza la vyama vya Siasa

Katibu huyo amesema, Khatibu amepata kura 126 na kura nne zilipigwa hapana.

Baada ya kutangazwa mshindi, Shubuda ambaye ni mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa nchini amesema, akishinda Urais wa Tanzania atahakikisha anaweka usawa kwa wananchi ikiwemo kuendesha shughuli za umma pasina upendeleo wa aina yoyote.

Naye, Khatibu amesema atahakikisha wanawake wanaoishi mazingira magumu hususan wanaopata mimba na wale wenye tabia za kuwakimbia waume zao anawashughulikia katika kipindi kifupi.

error: Content is protected !!