May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sheria ya kulinda data, faragha yaja

Spread the love

 

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, amesema maandalizi ya muswada wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, yako katika hatua ya mwisho kukamilika. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Nape ametoa kauli hiyo leo Jumatatu, tarehe 14 Machi 2022, jijini Dar es Salaam, akitaja mafanikio ya wizara yake ndani ya mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Waziri huyo wa habari, amesema utungwaji wa sheria hiyo unalenga kuvutia wawekezaji kwani itawahakikishia ulinzi wa taarifa zao.

“Lakini sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi (Privace Data Protection bill), iko kwenye hatua za mwisho kabisa. Tumeshafanya mchakato ndani ya mwaka mmoja. Hii sheria tunayo ni sheria ya muhimu sababu vinginevyo uwekezaji utakuwa mgumu,” amesema Nape.

Nape amesema, sheria hiyo haijatungwa kwa sababu ya kuibuka kwa matukio ya uvujaji wa sauti za mazungumzo ya watu yaliyofanyika kwa njia mbalimbali mitandaoni, bali imetungwa ili kulinda faragha za watu.

“Na kelele zimekuwepo za muda mrefu na ni kelele ya dunia, lazima tuwe na protection (ulinzi), sio kwa sababu kulikuwa na kurekodi rekodi watu hapa, hapana. Lakini ni kwa sababu ya kutunza privacy ya watu,” amesema Nape na kuongeza:

“Lakini dunia ndiko iliko, ukitaka watu waje wawekeze kwenye data, lazima kuwe na uhakika watu wako salama.”

error: Content is protected !!