November 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sheria ya bima ya ajali ipitiwe upya – Spika Tulia

Spread the love

SPIKA wa Bunge la Jamhuri, Dk. Tulia Ackson Mwansasu, ameitaka serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA), kuangalia upya utaratibu wa mashirika ya bima kuwalipa waathirika wa ajali nchini. Anaripoti Maria David … (endelea).

Alisema, kuna umuhimu wa kuwekwa utaratibu wa kisheria wa kuyalazimisha makapuni ya bima kulipa wahanga kwa haraka na sharti muda huo uelezwe kwenye sheria.

Dk. Tulia alitoa kauli hiyo, kwenye semina kuhusu usalama barabarani iliyoandaliwa kwa ajili ya wabunge na wizara ya mambo ya ndani ya nchi, iliyofanyika bungeni jijini Dodoma.  

Alisema Bunge liko tayari kusaidia kurekebishwa kwa sheria ya bima, iwapo itabainika kuwa ni muhimu kufanya hivyo.

Alisema, “…huwa sifurahi sana watu kusumbuliwa mahakamani, kwa mfano gari imeanguka na watu wamefariki au wamejeruhiwa sasa hawa watu wanahusika vipi na uzembe wa dereva.”

Alihoji, “kwanini bima zisiwalipe waathirika kwanza kisha ikaendelea na mambo mengine ya mahakamani kwa huyo mfanyabiashara?”

Akaongeza, “watu wa TIRA tusaidieni katika hilo na kama ni changamoto za kisheria sisi mtuletee tuifanyie kazi na haya yote ni lazima tubadili mtazamo; tunatamani haya mambo kuyatazama kwa upana sana.”

 

error: Content is protected !!