October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sheria Maudhui ya Mtandao kukatiwa rufaa

Nyundo ya Hakimu

Spread the love

MAHAKAMA Kuu, Kanda ya Mtwara leo tarehe 12 Juni 2019, imetoa kibali cha kukata rufaa ya kupinga Kanuni za Maudhui ya Mtandao ya Mwaka 2018. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Baraza la Babari Tanzania (MCT), Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Muungano wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu kwa pamoja waliomba kibali cha kukata rufaa mahakama hiyo kupinga matumizi mapya ya mtandao.

Katika kesi hiyo namba 25 ya mwaka 2018 ilifunguliwa na wadau hao wa habari, washtakiwa ni Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Mwanasheria Mkuu.

Akisoma hukumu katika Shauri la Maombi No. 5 la 2019 mbele ya Wakili Humphrey Mtuy, anayewakilisha jopo la mawakili wa waleta maombi na Wakili Wilbroad Ndunguru, akiwakilisha mawakili wa serikali, Jaji Dkt. Fauz Twaib amesema kuwa, pande zote mbili zimeonesha kutokuridhishwa na matumizi ya neno maudhui ingawa wamekuwa na hoja tofauti.

Na kwamba, maombi hayo yanahusisha watumiaji wengi wa mitandao walioathirika na uamuzi ya mwanzo wa kutumika kwa kanuni hizo.

Jajai Twalib ameridhia kuwa, maombi ya rufaa yapelekwe katika Mahakama ya Juu (Mahakama ya Rufaa) kwa ajili ya kusikilizwa na kutolewa uamuzi.

Awali, Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mtwara ilitupilia mbali shauri la kupinga matumizi ya kanuni za maudhui ya kimtandao.

Hukumu hiyo ilitolewa tarehe 9 Januari 2019 na Jaji Wilfread Ndyansobera. Jaji huyo alisema kuwa, maombi hayo hayakuwa na uzito.

error: Content is protected !!