
Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
SERIKALI imesitisha sherehe za kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).
Hayo amesema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akizungumza ofisini kwake jijini Dodoma leo tarehe 25 Aprili 2019.
Waziri Majaliwa amesema kiasi cha fedha Sh. 988.9 milioni ambazo zilitengwa kwa ajili ya sherehe hizo ambazo zilitarajiwa kufanyika tarehe 26 Aprili 2019, zimeokolewa na kwamba zitapangiwa matumizi mengine.
Waziri Majaliwa amesema tarehe 26 Aprili 2019 itakuwa ni siku ya mapumziko kwa ajili ya kuadhimisha muungano huo, na hakutakuwa na shamrashamra za aina yoyote ile.
More Stories
Mbowe ataja mambo mawili magumu ya JPM
CCM, wastaafu watakiwa kutubu
Chadema wabisha hodi Ikulu