Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Shekhe aonya wafanyabiashara kutopandisha bei za bidhaa Ramadhani
Habari Mchanganyiko

Shekhe aonya wafanyabiashara kutopandisha bei za bidhaa Ramadhani

Spread the love

 

SHEKHE wa Mkoa wa Dodoma, Mustapha Rajabu amewataka wafanyabiashara kutougeuza mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuwa wa kujitajirisha kwa kupandisha bei za bidhaa zao. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kiongozi huyo wa dini ametoa angalizo hilo leo tarehe 22 Machi, 2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuelekea mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Amesema iwapo wafanyabiashara watapandisha bei za bidhaa zao watawanyima haki wale wenye kipato kidogo cha kupata huduma zinazostahili wakati wa mfungo huo.

Shekhe amesema mwezi huo utumike kwa ibada kamilifu mbele za Mwenyezi Mungu ambapo ndani yake ni pamoja na kuwajali watu wenye kuhitaji misaada mbalimbali kama vile wajane, yatima, wazee, wafungwa na watoto waliozaliwa magerezani.

“Hivyo niwaombe wafanyabiashara hususani waumini wa dini ya kiislamu kuwa mwezi mtukufu wa ramadhani, usigeuzwe kuwa wa kujitajirisha bali watumie nafasi hiyo kuwaangalia pia wale wasiokuwa na uwezo wa kushiriki futari ili na wao waweze kushiriki” amesema.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Bakwata wilaya ya Dodoma, Bashiru Husseni amewataka mashekhe wa kata kutumia nafasi zao kuwaelimisha waumini umuhimu wa kujiandikisha kwenye sensa ya watu na makazi.

Amesema mashekhe wana nafasi kubwa ya kuwaelimisha waumini na wakajitokeza kuhesabiwa na serikali ikafikia malengo yao.

Aidha, amewataka vijana wa dini hiyo kuendelea kufanya kazi kwa bidii zenye tija zitakazowainua kiuchumi, badala ya kukaa kwenye makundi na kuinyoshea vidole kutokana na kukosa ajira.

Amesema fursa ziko nyingi ambazo wanaweza kujiingizia kipato, hivyo watumie nafasi hizo kwa kufanya kazi na siyo kuinyooshea vidole serikali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Gardner Habash wa Clouds Fm afariki dunia

Spread the loveALIYEKUWA mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

error: Content is protected !!