Monday , 30 January 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Shekhe ahukumiwa kwa kumwagia mtu majimoto
Habari Mchanganyiko

Shekhe ahukumiwa kwa kumwagia mtu majimoto

Spread the love

 

MAHAKAMA ya Wilaya imemhukumu Shekhe wa Mkoa wa Katavi, Mashaka Nassoro ‘Kakukulu’ kifungo cha miezi sita jela au kulipa faini ya Sh 50,000. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mpanda … (endelea).

Mshitakiwa amepewa adhabu hiyo baada ya Mahakama hiyo kumtia hatiani, kwa kosa la kumsababishia maumivu makali Asha Aman kwa kummwagia moto mwilini.

Akitoa hukumu hiyo juzi mjini hapa, Hakimu Gosphar Luoga alisema mshitakiwa alitenda kosa hilo kinyume cha sura 225 ya kanuni ya adhabu 16 ya mwaka 2021.

Hakimu Luoga alieleza kuridhishwa na ushahidi wa upande wa mashitaka ambao uliithibitishia Mahakama hiyo bila kuacha chembe ya shaka, kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo.

“Ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka haujaacha chembe ya shaka. Licha ya mshitakiwa kuwa kosa lake la kwanza, namuhukumu alipe faini ya Sh 50,000, akishindwa atumikie kifungo cha miezi sita jela,” Hakimu alisema katika hukumu yake.

Awali, ilidaiwa mahakamani hapo, kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Februari 28, mwaka jana mjini hapa.

Mahakama ilielezwa, kuwa siku ya tukio Asha alizozana na Mwajuma Haruna ambaye ni shemeji wa mshitakiwa wakiwa jikoni.

Katikati ya mzozo, mshitakiwa aliingia jikoni na kumtukana Asha, ndipo Shekhe akachukua chombo chenye maji ya moto na kummwagia Asha mwilini na kumsababishia maumivu na kisha kumkandamiza sakafuni, na katika jitihada za kujiokoa, Asha alimpiga mshitakiwa kwa chupa.

Upande wa mashitaka uliita mashahidi watatu kutoa ushahidi wao mahakamani hapo.

Ilielezwa kuwa tukio hilo liliripotiwa Polisi na Asha kupewa fomu namba 3 iliyomwezesha kutibiwa katika hospitali ya rufaa mkoa wa Katavi mjini hapa kwa wiki moja.

Akijitetea, mshitakiwa aliomba Mahakama imwachie huru, hata hivyo mshitakiwa aliepuka kifungo baada ya kulipa faini na kuwa huru.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chongolo asikitishwa na mradi wa Mil 900 kutoanza kutoa manufaa

Spread the loveKATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari Mchanganyiko

Huawei Tanzania yatajwa miongoni mwa waajiri bora kimataifa

Spread the loveKAMPUNI ya Huawei Tanzania imetajwa kuwa mwajiri bora nchini na...

Habari Mchanganyiko

Waziri wa uchumi wa Finland atua nchini, kuteta na mawaziri 7

Spread the loveWAZIRI wa Masuala ya Uchumi wa Finland, Mika Tapani Lintilä...

Habari Mchanganyiko

Asimilia 79 wafeli somo la hesabu matokeo kidato cha nne

Spread the loveWATAHINIWA wa shule 415,844 sawa na asilimia 79.92 ya watahiniwa...

error: Content is protected !!