July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sheikh wa Takbir ya ACT-Wazalendo akanwa kweupe

Spread the love

SHEIKH Juma Ramadhan, Imamu wa Msikiti wa Masjid Taqwa, jijini Dar es Salaam, amejipachika cheo kisicho chake. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Wakati akizungumza na waandishi wa habari jana tarehe 28 Machi 2018, kuhusu ufafanuzi wa matumizi ya neno ‘takbir’ lililotolewa na wanaotajwa kuwa wanachama wa ACT-Wazalendo, Sheik Ramadhan alijiita Naibu Amiri wa Shura ya Maimam Mkoa wa Dar es Salaam. 

Imebainika kwamba si kweli. Mwenye cheo hicho ni Sheikh Hassan Abass ambaye pia ni Amir wa Shura ya Maimam Mkoa wa Ilala.

Jana tarehe 27 Machi 2019 akizungumza katika mkutano wake na wanahabari jijini Dar es Salaam, Sheikh Ramadhani alilaani hatua ya chama cha ACT-Wazalendo kutumia Takbira katika shughuli zake za kisiasa huku akitoa vituko.

“Shura ya Maimamu Mkoa wa Dar es Salaam haijatoa fatwa kuhusu jambo hilo.

“Haijafanya hivyo kwa sababu haioni nia mbaya kwa waliofanya hilo.” Imeeleza taarifa iliyotolewa na Shura ya Maimam leo tarehe 28 Machi 2019 na kuongeza;.

“Sheikh Juma Ramadhan si Naibu Amiri wa Shura Mkoa wa Dar es Salaam,  Naibu wa Ashura Mkoa wa Dar es Salaam anaitwa Hassan Abass ambaye pia ni amiri wa Shura ya Maimamu wilaya ya Ilala na Imamu Mkuu wa Msikiti wa Ijumaa Gongo la Mboto,.”

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, jumuiya hiyo haifungamani na chama chochote cha siasa.

“Sisi hatufungamani na chama chochote kwani tunafahamu kwamba, waumini wa dini ya kiislamu wanashiriki katika vyama mbalimbali vya siasa.

“Kwa taarifa hii shura ya Mamaimamu Mkoa wa Dar es Salaam haihusiki na yale yote yaliyozungumzwa na Sheikh Juma Ramadhani katika mkutano wake na vyombo vya habari.”

error: Content is protected !!