August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sheikh Said: Kuweni na huruma

Spread the love

AHMED Said, Kaimu Shekh wa Mkoa wa Dodoma, Baraza Kuu la Waislamu (Bakwata) amewaomba wafanyabiashara kuwa na huruma, anaandika Dany Tibason.

Pia amewataka kuwa na hofu ya Mungu na kwani hawapaswi kupandisha bei ya vyakula wakati wa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Mbali na hilo amewataka wafanyabiashara ambao wanauza sukari, kushusha bei ya bidhaa hiyo muhimu kwani katika kipindi hiki inatumiwa zaidi.

Rai hiyo imetolewa na Ahmed Said, Kaimu Shekh wa Mkoa wa Dodoma, Baraza Kuu la Waislamu (Bakwata) Mkoa wa Dodoma.

‘’Mahitaji ya sukari ni makubwa katika mfungo wa Ramadhan kuliko wakati wowote, niwaombe pia katika hili wafanyabiashara wasiifiche sukari,’’ amesema Shekh Said.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Shekh wa Mkoa wa Dodoma, Ahmed Said aliwataka wafanyabiashara kutopandisha bei ya bidhaa muhimu ambazo msimu huu wa mwezi wa Ramadhani utumiwa zaidi.

Shekh Said amewataka wafanyabiashara kuwa na hofu ya Mungu zaidi na kutambua kuwa, kipindi hiki ni muhimu kwa kufanya toba.

“Wafanyabiashara wasidhani kuwa watakapopandisha bei bidhaa watakuwa wamenufaika kwani wanatakiwa kutambua kuwa, uchumi ni mgumu kwa sasa na wapo watu ambao watakuwa wananung’unika kwa kukosa huduma muhimu, manung’uniko ya watu hao ni sehemu ya laana kwa wafanya biashara hao,” amesema Shekh Said.

Amesema kuwa, wafanyabiashara watambue kwamba, licha ya kufanya biashara lakini wanatoa huduma kwa jamii na Mungu anatambua huduma yao na kupitia huduma hiyo atawabariki zaidi,” amesema Shekh Said.

“Kabla ya Mwezi wa Ramadhani bei za vyakula ilikuwa nzuri ila sasa watapandisha, nawaomba wawe na huruma na wamwogope Mwenyezi Mungu katika mwezi huu,’’ amesema Shekh Said.

Katika hatua nyingine amewataka wenye magari ya kusafirishia mizigo ambao wanatoa baadhi ya vyakula mashambani kutowapandishia bei wafanyabiashara.

‘’Wenye magari wasione huu ndio mwezi wa kuchuma kwani  husingizia kuwa gharama za kusafirisha ni kubwa, na wao niwaombe wapunguze bei,’’ amesema.

 

error: Content is protected !!