January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sheikh Ponda: Wananchi hawana maamuzi ya kisiasa

Spread the love

KATIBU Mkuu wa Shuraa ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, amesema tatizo la wananchi kutokuwa na uhuru wa kufanya maamuzi ya kisiasa bado lipo kama ilivyokuwa wakati wa ukoloni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Sheikh Ponda ameyasema hayo leo Jumanne, tarehe 7 Desemba 2021, katika dahalo wa uchambuzi wa kitabu cha Mwandishi wa habari mkongwe nchini, Jenerali Ulimwengu, jijini Dar es Salaam.

“Ule uhuru haukuwepo kwa wananchi kwa sababu uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa haikuwepo, kwa maana hiyo tatizo linaonekana ni lilelile labda linapata taswira tofauti, lakini linaendelea toka wakati wa ukoloni mpaka sasa,” amesema Sheikh Ponda.

Akichambua kitabu hicho chenye jina la Rai ya Ulimwengu, Sheikh Ponda amesema kimeelezea namna maamuzi ya kisiasa ya wananchi yalivyofungwa katika vyama vya siasa.

“Kabla ya wakoloni uhuru wa ksiasa ulishikwa na wakoloni, sisi Waafrika hatukushika maamuzi ya kisiasa, baada ya uhuru matarajio makubwa yalikuwa tutashika yale maamuzi ya kisiasa,” amesema

Sheikh Ponda na kuongeza; “Lakini kwa mujibu wa makala, zilikuwa zinaonesha baada ya uhuru kuna maamuzi ya kisiasa yakafungwa, vilevie na ya wanachi yakafungwa na vyama vya siasa, kwamba ukitaka kufanya siasa lazima uende kwenye vyama.”

error: Content is protected !!