February 28, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Sheikh Ponda kimenuka, apewa siku tatu kujisalimisha Polisi

Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa. Picha ndogo Sheikh Ponda Issa Ponda

Spread the love

JESHI la Polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam limemtaka Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, Sheikh Issa Ponda kujisalimisha mikononi mwa Polisi ndani ya siku tatu kuanzia leo, anaandika Hamisi Mguta.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema Sheikh Ponda ametenda makosa ya jinai likiwamo la uchochezi, lakini pia amekuwa akitoa lugha ambazo ni za kejeli dhidi ya serikali.

“Kukimbia hakutamsaidi, hao tuliowakamata wamehojiwa na wameachiwa kwa dhamana, unajitia mtumwa wa kukimbia bila sababu aje aripoti kwenye ofisi ya ZCO ili aweze kuhojiwa ndani ya siku tatu vinginevyo hatakuwa salama,” amesema Mambosasa.

Jana Sheikh Ponda alinusurika kutiwa nguvuni baada ya polisi kufika katika hotel ya Iris iliyopo Kariakoo muda mfupi alipomaliza mkutano wake na waandishi wa habari.

Hata hivyo, polisi walimkosa Sheikh Ponda na kuishia kuwakamata waandishi wa habari na kuondoka nao.

Sheikh Ponda alifanya mkutano huo kwa lengo la kutaka kueleza safari yake ya kumtembelea Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Tundu Lissu aliyepigwa risasi na watu wasiofahamika tarehe 7 Septemba mwaka huu akiwa mjini Dodoma.

error: Content is protected !!