January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sheikh Ponda huru

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Morogoro imemwacha huru Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda aliyekuwa akituhumiwa kwa makosa ya uchochezi. Anaandika Yusuph Katimba … (endelea).

Hakimu Mfawidhi wa Mkoa wa Morogoro, Mary Moyo amefikia uamuzi huo baada ya kuonesha kutoridhishwa na upande wa mashtaka na hivyo kuonekana hana hatia.

Sheikh Ponda alifikishwa mahakamani Agosti 2013 kukabiliwa na kesi ya jinai Na.128/2013 akidaiwa kutoa kauli za kichochezi na zilizoonekana kuumiza imani ya dini nyingine.

Mara kadhaa mahakama hiyo imekuwa ikiahirisha hukumu hiyo kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na hakimu kuwa nje ya mkoa huo pamoja na matatizo ya afya.

Mara ya mwisho kesi hiyo iliahirishwa kutolewa hukumu Novemba 18, mwaka huu baada ya Hakimu Moyo aliyetarajiwa kutoa hukumu hiyo kuwa nje ya Mkoa wa Morogoro kikazi.

Taarifa hiyo ilionekana kuwaudhi watu waliokuwa wamekusanyika katika eneo la mahakama hiyo waliokuwa na shauku kubwa ya kujua hatima ya kiongozi huyo.

Hati ya mashitaka ya kesi ya Sheikh Ponda ilikuwa na jumla ya mashitaka matatu lakini Julai 22 mwaka huu, Hakimu Moyo alitoa uamuzi wa kumfutia shitaka la kwanza kwasababu lilitolewa uamuzi na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, na hivyo mahakama hiyo ya Morogoro siku hiyo ilitoa uamuzi wa kumuona ana kesi ya kujibu katika mashitaka mawili yaliyosalia ambayo ni kosa la pili na la tatu.

error: Content is protected !!