Friday , 3 February 2023
Habari MchanganyikoTangulizi

Sheikh Ponda gizani tena

Sheikh Issa Ponda, Katibu wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu
Spread the love

MAHAKAMA ya Rufaa, jijini Dar es Salaam leo tarehe 4 Julai 2019 imefuta hukumu ya Sheikh Ponda Issa Ponda, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini iliyotolewa tarehe 9 Mei 2013 katika Mahakama ya Kisutu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Katika kesi hiyo ya jinai No. 245 ya 2012, Sheikh Ponda na wenzake walishtakiwa kwa madai ya kuvamia kiwanja cha Markazi, Chang’ombe mali ya Waislam akidai kimeuzwa kifisadi na Baraza Kuu la Waislam (Bakwata).

Hakimu Victoria Nongwa wa Mahakama ya Kisutu, alimhukumu Sheikh Ponda kifungo cha nje cha miezi 12 huku washtakiwa wengine kwenye kesi hiyo waliachwa huru.

Hata hivyo, Sheikh Ponda kupitia jopo lake la mawakili, alikata rufaa Mahakama Kuu kupinga yeye kutiwa hatiani kwasababu, hukumu haikuzingatia ukweli kuwa, alisimamia madai halali ya Waislamu.

Rufaa hiyo No. 89 ya 2013, ilisikilizwa na Jaji Shangwa ambapo tarehe 27 Novemba 2014, jaji huyo aliifuta hukumu ya Kisutu kwamba, Sheikh Ponda hakuwa na hatia yoyote.

Kutokana na uamuzi huo, Jamhuri haikuridhika hivyo iliamua kukata rufaa No. 57 ya 2015 kwenye Mahakama ya Rufaa Tanzania chini ya majaji watatu; Stella Mugasha, Fredrick Wambali na Rehema Kerefu.

Akisoma uamuzi wa mahakama hiyo leo, Msajili Amiri Msumi amesema, mahakama hiyo imefuta hukumu ya Mahakama ya Kisutu iliyomuhukumu Sheikh Kifungo cha nje cha miezi 12.

Pia mahakama hiyo imefuta hukumu ya Mahakama Kuu iliyomfutia Sheikh Ponda kifungo cha nje cha miezi 12 kwa hoja kuwa, hukumu zote mbili ni batili kutokana na kutofuata sheria.

Kutokana na hatua hiyo ya Mahakama ya Rufaa, kesi hiyo imerejeshwa upya katika Mahakama ya Kisutu ili kumtia hatiani na kisha kutoa adhabu upya.

Kwamba, wakati rufaa ikianza kusikilizwa, iligundulika kuwepo kwa kasoro ya kisheria katika hukumu ya Mahakama ya Kisutu ambapo Hakimu Nongwa aliandika hukumu yake kinyume na matakwa ya kisheria, yaliyo katika kifungu cha 235(1) cha sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.

Kwamba, Hakimu Nongwa alitoa hukumu ya kifungo cha nje bila ya kwanza kumtia hatiani mshitakiwa (sentence without conviction).

Baada ya kugundulika kasoro hiyo, upande wa Jamhuri walitaka hukumu ifutwe lakini faili lirudishwe Kisutu ili mahakama ikamtie hatiani upya.

Uamuzi huo umeibua mvutano mahakamani hapo baada ya Wakili wa Sheikh Ponda, Juma Nassoro kudai kuwa, mteja wake hawezi kutumikia adhabu mbara mbili kwa kosa moja.

Wakili Nassor ameiambia mhakama hiyo kuwa, kisheria hukumu ilishatolewa na Sheikh Ponda ametumikia adhabu, hivyo kurudisha faili Kisutu ili ahukumiwe upya, haitakuwa haki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NMB yafadhili ziara ya mafunzo machinga, bodaboda Dar nchini Rwanda

Spread the loveBENKI ya NMB imefadhili ziara ya siku nne ya mafunzo...

ElimuHabari Mchanganyiko

Waliopata Division one St Anne Marie Academy waula, Waahidiwa kupelekwa Ngorongoro, Mikumi

Spread the love WANAFUNZI wa shule ya St Anne Marie Academy waliofanya...

Habari Mchanganyiko

Wadau wataka kasi iongezeke marekebisho sheria za habari

Spread the love  WADAU wa tasnia ya habari wametakiwa kuongeza juhudi katika...

Habari Mchanganyiko

TEF yawatuliza wadau wa habari marekebisho vifungu kandamizi

Spread the love  JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF), limewataka wadau wa habari...

error: Content is protected !!