March 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Sheikh Ponda atii sheria bila shuruti, ajisalimisha Polisi

Sheikh Ponda, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Taasisi za Kiislam Tanzania

Spread the love

SHEIKH Issa Ponda, Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania amethibitisha kuwa anaheshimu mamlaka na sheria kutokana kutii wito wa Jeshi la Polisi, anaandika Faki Sosi.

Sheikh Ponda amewasili Kituo kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam majira ya saa nne asubuhi.

Wito huo ulitolewa Jana na Kamanda wa Polisi Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo alimpa siku tatu kujisalimisha kituoni hapo.

Juzi Jeshi la Polisi lilivamia mkutano uliofanywa na Sheikh Ponda na waandishi wa habari kwenye Hotel ya Iris jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumtia mbaroni.

Hata hivyo Polisi walimkosa Sheikh Ponda.

error: Content is protected !!