Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Sheikh Ponda ataka misingi imara itakayosaidia vyombo vya habari kupumua
Habari Mchanganyiko

Sheikh Ponda ataka misingi imara itakayosaidia vyombo vya habari kupumua

Sheikh Issa Ponda, Katibu wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu
Spread the love

 

KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda, ameishauri Serikali iweke misingi imara itakayosaidia kujenga uhuru wa kudumu wa sekta ya habari kutekeleza shughuli zake bila vikwazo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Sheikh Ponda ametoa ushauri huo leo tarehe 16 Januari 2023, akizungumza na wanahabari kuhusu mchakato wa marekebisho ya sheria zinazosimamia sekta ya habari, unaofanywa na Serikali kwa kushirikiana na wadau.

“Nashauri viongozi kuhakikisha wanaweka misingi imara ili tasnia iepukane na hali ya sheria ambazo zinapunguza uwezo wao wa kufanya kazi kama sheria kandamizi ambazo zimejitokeza huko nyuma. Aweke misingi imara kuhakikisha anmgalau sekta ya habari inapumua kutokana na mazingira yaliyojitokeza kwenye maeneo mengi,” amesema Sheikh Ponda.

Akizungumzia manufaa ya vyombo vya habari kuwa huru, Sheikh Ponda amesema itasaidia kuaminika kwa umma kwa kuwa vitawasilisha taarifa kwa usahihi, pamoja na ksuaidia Serikali na sekta binafsi kutathimini shughuli zao za kila siku.

“Uhuru wa vyombo vya habari faida yake ya kwanza ni malengo ya kuanzishwa chombo cha habari yatakuwa yamefikiwa kwa sababu bila shaka chombo cha habari kinatakiwa kiwe huru. Lakini pia vikiwa huru vitaaminika kwa umma maana yake vitaeleza au vitawasilisha zile fikra za umma kwa usahihi kwa maana hiyo chombo kitaaminika kwa umma,” amesema Sheikh Ponda.

Kiongozi huyo wa dini amesema “yale matakwa ya wananchi au ukosoaji yatafikiwa, lakini vikiwa huru vitasaidia kusambaza elimu inayohitajika katika jamii. Vitasaidia mataifa ya nje kufahamu hadhi ya taifa lao, uchumi wao na hali ya kisiasa ikoje kiasi kwamba watu wa mataifa mengine watajipanga kuleta ushirikiano mzuri sababu watakuwa wanafahamu vizuri ile hali ya taifa.”

Aidha, Sheikh Ponda amesema demokrasia ikiimarika itasaidia kuimarisha utendaji wa vyombo vya habari.

“Ikiwa kuna demokrasia vyombo vya habari vitakuwa hai, maana yake sheria zitakuwa nzuri sio zile za ukandamizaji sababu kinyume na demokrasia ni udikteta yaani mabavu, kwamba watu hawapati uhuru wa kuzungumza, kukosoa na kadhalika,” amesema Sheikh Ponda.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love  MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awalilia 17 waliofariki ajalini wakisafirisha maiti

Spread the love  RAIS Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa...

Habari Mchanganyiko

Wanawake wachimbaji wajenga zahanati kuokoa afya za wakazi 2000

Spread the love  ZAIDI wakazi 2,000 wa kijiji cha Nyamishiga Kata ya...

Habari Mchanganyiko

Baada ya Congo DR, Somalia mbioni kujiunga na EAC

Spread the love  TAIFA la Somalia liko mbioni kuwa mwanachama rasmi wa...

error: Content is protected !!