September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sheikh Ponda ataja sifa za wagombea uchaguzi mkuu

Sheikh Ponda Issa Ponda (katikati)

Spread the love

SHEIKH Ponda Issa Ponda, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, ametaja sifa za wagombea katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 9 Julai 2020, jijini Dar es Salaa amesema, waraka wa taasisi hiyo uliotolewa leo umeorodhesha sifa ambazo mgombea kwenye ngazi mbalimbali anapaswa kuwa nazo.

Ametaja sifa zilizoelezwa kwenye waraka huo kuwa ni:-

1. Mgombea awe mkweli na mwenye utu.

2. Awe mwenye kuheshimu kiapo.

3. Awe mwenye sifa ya kupiga vita ubaguzi wa aina zote.

4. Awe na elimu kubwa au wastani, mwenye maarifa ya kutosha ya kuongoza watu na serikali.

5. Awe mtu mwenye mtazamo wa maendeleo kwa Taifa na Watanzania wote.

6. Awe mwenye kuheshimu Uhuru wa Mawazo ya watu wengine.

7. Awe mwenye kuzijua Haki za binaadamu na kuzilinda.

8. Asiwe mwenye kutumia vibaya madaraka na kuvunja sheria za nchi.

9. Awe ni mwenye kupenda Umoja wa Taifa na dhamira ya Muungano wa kweli.

10. Asiwe fisadi na mwenye kuficha ukweli.

11. Awe mwenye kumtambua Mwenyezi Mungu wa Walimwengu wote.

12. Asiwe kibri, dikteta mkandamizaji na mdhalilishaji wa watu anaowaongoza.

13. Asiwe mtu mwenye kujali maslahi yake na kundi lake sambamba na kufikiria sheria za kujilinda dhidi ya mkondo wa sheria kwa tuhuma za ufisadi na uvunjaji wa Haki za Binadamu.

error: Content is protected !!