January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sheikh Khalifa awaweka sawa Waislam

Spread the love

WAISLAM nchini wametakiwa kutunza amani kwa kuendelea kufanya mambo mema na kuachaa mambo ambayo yatapelekea kuchochea vurugu katika jamii. Anaandika Aisha Amran…(endelea).

Wito huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Taasisi ya Kislamu ya Imam Bukhari Foundation, Shekh Khalifa Khamisi wakati wa semina iliyowakutanisha waumini wa dini hiyo, yenye lengo la kujadili changomoto zinazowakabili Waislamu nchini na duniani kwa ujumla.

Shekh Khamis amesema, kwa sasa Waislamu wamekuwa wanafanya mambo ya kumkera Mwenyezi Mungu kwa kuwafanyia wenzao mambo maovu na kwamba matendo hayo hayaendani na mafundisho ya dini hiyo.

Amesema mafundisho ya dini hiyo yanaelekeza Waislamu kuwa na upendo kwa watu wote ndani ya jamii, kusaidiana pamoja na kuelekezana na kufanya mambo ya maendeleo.

Amefafanua kuwa, kwa sasa watu wengi wamekuwa wakihusiha masuala ya ugaidi yanayotokea duniani na dini hiyo jambo ambalo analipinga kwa kusema kuwa watu wanaofanya vitendo hivyo sio Waislam safi kwa kuwa dini hiyo haifungamani na ugaidi.

Hata hivyo Shekh Khamis amesema, kwa sasa nchini kumekuwa na mgawanyiko kati ya Waumini wa Dini ya Kiislamu na Serikali ambapo amedai sababu hiyo imetokana na hatua ya serikali kuwakamata viongozi wa dini hiyo.

“Katika semina hii tumekutana na waumini wa dini hii ili kurudusha upendo katika jamii ya Waislam nchini na serikali maana baadhi ya Waislam waliiwekea chuki serikali na leo tumetumia nafasi hiyo kuwataka kuondokana na hali hii na kuachia vyombo vya mahakama ndio vitenda haki,” amesema Shekh Khamis.

Kwa upande wake Shekh Hemed Jalala kiongozi wa kiroho wa dhehebu la Shia Ithna-sheri ya Tanzania ambaye naye alikuwa mchangia mada katika semina hiyo, amesema Waislamu kuendeleza kufanya mambo mema yatakayomfurahisha Mtume Muhammad (S.A.W) kwa kusema ndio njia pekee ya kuendana na dini hiyo.

error: Content is protected !!