August 5, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Sheikh Jalala: Funga hii iwe darsa kwetu

Spread the love

WAISLAM wameyakiwa kuifanya funga ya mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan kuwa ni darasa kubwa la huruma na mabadiliko ambalo yataleta amani na utulivu ndani ya nchi, anaandika Aisha Amran.

Haya yamesemwa leo na Sheikh Hemed Jalala, Kiongozi wa Chuo cha Kiislam cha Hawaza Imam Swadiq, Madhehebu ya Shia Ithna Sherri nchini wakati akizungumzia juu ya kuukaribisha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Amesema, katika mwezi wa Ramadhan huruma ambayo itakuwa moyoni mwa Waislam kwa kuwaangalia hali za wanyonge, walemavu, mayatima, wajane, wasiojiweza itakuwa ndio msingi wa kujenga imani.

Sheikh Jalala amesema, moja ya somo la funga ni kuwasaidia watu wasiojiweza iwe wa Dini ya Kislam au wasio Waislam na kwamba, kwa kufanya hivyo kunajenga uhusiona mzuri kwa Watanzania na kuleta amani na utulivu.

“Swaumu zetu hazitokamilika  kama hatutofanya mambo haya ya kuwasidia watu wenye matatizo mbalimbali,” amesema Sheikh Jalala.

Sambamba na hayo pia amesema, wanalaani vikali vitendo vya kinyama  vilivyotokea vya watu  kuuawa  kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana  katika mikoa mbalimbali nchini.

Amesema, anasikitika kuona Tanzania  nchi ambayo ina sifa ya amani na  utulivu yenye muunganiko wa dini mbalimbali na  haki ya  kuabudu kwa kila dini bila pingamizi, kufikia hatua ya kujiingiza katika  vitendo vya kinyama, ukatili na uvunjwaji wa amani.

Sheikh Jalala amesema mauaji yaliyotokea  Mwanza havina mahusiona na uislamu kwasababu uislam ni dini ambayo inalingania amani,maelewano  na huruma.

Pia amewataka watanzania kutokujihusisha na vitendo vya ugaidi na ukatili ambavyo vitapelekea  uvunjwaji wa  amani na utulivu wa nchi.

error: Content is protected !!