Saturday , 3 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Sheikh Dodoma: Vijana changamkieni fursa Mtumba
Habari Mchanganyiko

Sheikh Dodoma: Vijana changamkieni fursa Mtumba

Sheikhe wa Mkoa wa Dodoma, Mustapha Rajabu
Spread the love

SHEIKHE wa Mkoa wa Dodoma, Mustapha Rajabu amewataka vijana kutumia nguvu zao wakati serikali ikijenga mji wa kiserikali katika eneo la Mtumba, jijini humo. Anaripoti Danson Kaijage…(endelea).

Hatua hiyo imekuja kufuatia ujenzi wa majengo ya wizara mbalimbali katika mji wa kiserika katika eneo la Mtumba kusuasua kutokana na kukosekana kwa vibarua wa kusaidiana na mafundi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jana jijini humo tarehe 18 Machi 2019 Sheikhe Rajabu amesema, vijana ndio wenye nguvu hivyo wanatakiwa kujitokeza kwa wingi katika eneo la Mtumba kwa ajili ya kujenga majengo hayo.

“Ni aibu kusikia kwamba vibarua wanakosekana, niwaombe vijana popote walipo waende wakachape kazi kwani pia na ujira kwani kwa kufanya hivyo, watakuwa wameingia katika historia kwamba na wao walichangia katika ujenzi wa Makao Makuu,”amesema.

Aidha Sheikh Rajabu amewataka wakazi wa Dodoma kuwekeza katika maeneo mbalimbali kutokana na ujio wa Makao Makuu pamoja na serikali kuhamia mkoani humo.

“Baadaye tusije tukaanza kulalamika kwamba tumesahaulika, wakati ndio huu mwenye uwezo wa kuwekeza kwenye chakula afanye hivyo, mwenye uwezo wa kuwekeza katika majengo muda ndio huu hizi ni fursa ni lazima tuzifanyie kazi,”amesema Sheikh Rajabu.

Pia amewataka wakazi wanaohamia jijini humo kujikita kumcha mwenyezimungu pamoja na kufanya mambo ambayo yanampendeza ikiwemo kujenga misikiti ya kutosha.

“Watu wanaongezeka, Dodoma inazidi kuwa kubwa hivyo ni lazima na misikiti ijengwe kwa wingi, nawaomba hawa wanaohamia watusaidie tujenge misikiti mipya kwani watu wanazidi kuwa wengi,”amesema.

Pia amewataka Waislamu kuutumia mwezi wa Rajabu kuwa karibu na familia pamoja na kuhakikisha watoto wa kiislamu wanapata elimu zote ya dunia na ya dini.

“Elimu ndio kila kitu waislamu tusimamie kuhakikisha watoto wetu wanapata elimu ya dunia na ile ya Dini ya Kiislamu ili waweze kumwogopa Mungu,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Magunia 731 ya bangi yakamatwa, mamia ya hekari yateketezwa Arumeru

Spread the love  MAMIA ya magunia ya madawa ya kulevya aina ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Bosi NIC apandishwa kizimbani, akabiliwa na mashitaka 365

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa...

Habari Mchanganyiko

Serikali yakabidhi eneo la mahakama ya Afrika ya haki za binadamu

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa...

Habari Mchanganyiko

Udhamini wa NMB mikutano ya ALAT wafikia 1.2 bilioni

Spread the loveBENKI ya NMB imeendelea kufanya kazi kwa karibu na Asasi...

error: Content is protected !!